Social Icons

Saturday, 13 September 2014

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni awasili nchini kwa ziara ya siku moja.

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiteremka katika ndege iliyomleta leo jijini dar es Salaam kwa ajili ya  ziara yake ya siku moja nchini Tanzania .
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuwasili  leo jijini  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja.
 Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa  Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia ngoma za utamaduni baada ya kuwasili  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa  Mwalimu Julius  Nyerere Leo jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya ziara ya siku moja hapa nchini.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Katikati)akipata maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na kushoto ni  Rais wa  Uganda Yoweri Museveni  ambaye amewasili nchini leo  kwa ajili ya ziara ya siku moja . ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
 Ndege iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa  Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

 
 
Blogger Templates