Social Icons

Thursday, 29 January 2015

Hadithi: Familia tata - 15


“Kaka Festo nina shida kubwa na wewe na ndicho nilichokuitia,” Asfat alisema. Festo akabaki kimya, akiwa na hamu kubwa ya kusikia alichoitiwa, akatingisha kichwa kuashiria aendelee kuzungumza.
“Najisikia kukupenda, nataka uwe mpenzi wangu,” Asfat alisema, akiwa amemkazia sura Festo. 

Whaat?” Festo aliuliza kwa mshangao! Sasa endelea..

“Hujanisikia kaka Festo? Nakupenda, nataka uwe mpenzi wangu,” Asfat alirudia tena kumwambia kijana aliyekuwa amekaa mbele yake, ambaye kiumri ni mkubwa kwake kwa miaka mitano.
Festo akamtazama vizuri Asfat, ni binti mrembo kuliko wasichana wengi aliowahi kutoka nao, lakini siku zote amekuwa dada yake. Alikuwa ni swahiba mkubwa wa marehemu mdogo wake, Juddy.

Ni dada yake kabisa, anakijua hadi chumba anacholala nyumbani kwao,  anamjua kila mtu kwao, ameingia kila chumba nyumbani kwao, anawajua ndugu zake wote..!!
“Kwa nini Asfat?” Festo, baada ya kumtazama huku akitafakari kwa muda mrefu, alimuuliza.
“Basi tu, imetokea. Najua unajiuliza maswali mengi sana, hata mimi nilijiuliza kabla ya kupata ujasiri wa kukuambia kaka,” Asfat alimwambia Festo.

“Dada nadhani iwe hapana, unanijua vizuri kaka yako, sina kawaida ya kutulia na msichana mmoja, mimi bado kijana, siwezi kuruhusu nikufanyie hivyo wewe.” “Utatulia tu, mimi niko hot kaka, utanipenda, lakini hata kama hautatulia, sitajali, kwa sababu nimeamua kukupenda nikijua wazi jinsi ulivyo, usijali,” Asfat alimwambia kaka yake.

Festo alicheka sana, akaagiza bia ingine kwa ajili ya Asfat, akaagiza na mishikaki kadhaa. Asfat hakuelewa kama ombi lake lilikubaliwa au la, lakini kwa kuwa alimfahamu jirani yake huyo kama mtu wa kinywaji, alijua atalipata jibu, tena zuri, kabla hawajaondoka.

Festo akazama katika mawazo. Hakuwahi kufikiria hata siku moja kama angeweza kuwa kimapenzi na Asfat, siyo tu kwa sababu alikuwa rafiki wa karibu sana wa mdogo wake, lakini pia alikuwa ni kama dada yake wa kuzaliwa. Tokea kukua kwao, wameishi kama ndugu. Leo awe mpenzi wake, wataeleweka? Moyo wake ukakataa.

Akamtazama vizuri msichana aliyekuwa mbele yake, alivutia kwa kweli. Kifua chake kilijaa vizuri, sura yake ilitulia na kwa hakika, alikuwa na figa nzuri mno kwa viwango vya Festo. Lakini kitu flani ndani ya nafsi yake, kilikataa kabisa wazo la kuruhusu hisia za kimapenzi.

Asfat alikuwa akimtazama Festo kwa jicho la huba usoni, lakini ndani ya moyo wake alimchukia kupita kiasi, alidhamiria kumuangamiza kwa namna yoyote. Alizijua tabia za walevi, hata kama alijifanya kutomtamani kwa sasa, baadaye angebadilika tu, hivyo akavuta subira na kuzidi kuinywa kwa fujo bia yake ili iishe, aagize nyingine.

Wakahamia katika stori zingine za kimaisha, wakazungumza sana huku wakiongeza kinywaji, Ndovu na Konyagi. Taratibu zikaanza kupanda, kwa makusudi kabisa, Asfat akamshauri kaka yake wahamie katika kibanda kilichokuwa bila taa, akidai mwanga unamfanya alewe haraka.

Ilikuwa sababu ambayo Festo aliielewa na kuikubali, wakahamia sehemu nyingine yenye giza, wakakaa, viti vyao vikiwa karibu zaidi!
Waliendelea kunywa, Asfat katika bia yake ya sita, akajikuta akishindwa kuvumilia, akapeleka mkono wake katika kifua cha Festo, ambaye sasa mzinga wake wa pili ulikuwa unakaribia nusu.

Festo alipenda kufunga shati lake hadi kifungo cha juu kabisa, msichana huyo akafungua vifungo viwili, kisha akauingiza mkono wake na kuanza kuchezea nywele chache zilioota kifuani. Kijana wa kiume alimtazama akiwa haamini kama binti ambaye kwa miaka yote amekuwa dada yake, alidhamiria tendo lile ovu.

“Festo,” aliita kwa sauti ndogo, iliyojaa mahaba!
“Sema,” Festo aliitikia huku akiupeleka mkono wake katika kifua, akabonyeza bonyeza mara kadhaa na kujikuta akivutiwa nayo.

“Hujanijibu ombi langu, nakupenda sana kaka Festo, tafadhali nikubalie, usifikirie kuhusu watu watasemaje, haya ni maisha yetu mimi na wewe,” alisisitiza!
“Hebu punguza munkari mtoto mzuri, mbona una haraka?” Festo alimwambia Asfat, ambaye kwa maneno hayo akajisogeza karibu zaidi, sasa wakawa wanapumuliana.Hadithi

No comments:

 
 
Blogger Templates