Kwa akili ya harakaharaka waliamua kuita bajaji ya mmoja wa madereva wa pale kichochoroni ambao nao walikuwa wakiingiza kipato chao kupitia machangudoa wa maeneo hayo kwa kuwasafirisha wateja wa biashara hiyo kutoka sehemu moja hadi nyingine.
“Huu msala unajua!” alizungumza yule dereva kwa hamaki baada ya kuambiwa kinachoendelea kuhusu yule mzee aliyezirai ghafla baada ya kupewa penzi na Joy.
“Wewe kazi yako ni kumtupa tu huyu mzee mtaroni, kwani kuna ugumu?” alisema Joy kwa woga.
“Nipe elfu ishirini,” aliongea yule dereva.
“Jamani punguzapunguza kidogo hapa ndiyo kwanza nilikuwa naanza kazi, kaka angu,” alibembeleza Joy.
“Aah sista hiyo haipungui kabisa, hii kesi,” “Kaka angu, naomba basi upokee hii, nisaidie kama mdogo wako,” alizidi kubembeleza Joy, akatoa shilingi elfu 15 huku chozi likimtoka.
Yule dereva alimuonea huruma lakini alimpa sharti la kwenda naye hadi sehemu yenye mtaro ili kumtupa yule mzee huyo maana yule dereva alikuwa na wasiwasi kama msala utatokea.
Joy na dereva kwa kificho walimbeba yule mzee na kumuweka kwenye siti ya nyuma ya bajaji, wakamkalisha upande wa kutokea, mwenyewe Joy akiwa amemshikilia kiuno ili asidondoke.
Wakakata mitaa na kutafuta sehemu nzuri wamtupe, bahati nzuri maeneo mengi yalikuwa hayana watu kutokana na muda kwenda sana.
Dereva na Joy wakamshusha yule mzee ambaye bado alionekana kulegea vilivyo, wakamtelekeza pembezoni mwa barabara kisha wakageuza na kuondoka.
Wakiwa umbali wa mita kadhaa Joy aligeuka na kutazama kupitia kioo cha nyuma, akashtuka, akajikuta ameshika mikono kichwani
Huwezi amini yule mzee ambaye muda mchache uliopita alionekana amezirai, alionekana amesimama na kukimbia tena huku akiwa anacheka kwa sauti; “hahaa uroda burebure.”
Ni wazi kuwa Joy alikuwa ameingizwa mjini na yule mzee ambaye alijifanya amezimia baada ya kufanya naye mapenzi, kumbe lengo lake lilikuwa ni kutolipa hela yoyote baada ya huduma ya ngono.
Wakati yule dereva bajaji akiwa akicheka nusura mbavu zivunjike kwa tukio lile, Joy alikuwa amekasirika kiasi cha kutosha, hasira zilimpanda kwa hasara aliyokuwa ameingia; kwanza ametumika mwili wake bure pasipo kupewa chochote, cha pili alikuwa amelipia elfu 15 nzima ya bajaji kwa ajili ya kuutupa mwili wa mtu aliyedhani amezimia kumbe alikuwa ni tapeli.
Kwa huruma yake yule dereva bajaji aliamua kumrudishia shilingi elfu 10 Joy na kuchukua elfu 5 akamrudisha pale kichochoroni kwa machangu wenzake ambao mpaka muda huo wengine walikuwa wameshaenda na wateja zaidi ya mara tatu na kuingiza mkwanja wa kutosha.
Kwa hasira Joy akaagiza kinywaji kikali cha Kiroba vipakiti vitatu na kuvinywa harakaharaka. Vikamshusha hasira na kubust upya mudi yake.
Akasimama na kutega ndoano yake tena kwa mpita njia mmoja, kijana mtanashati aliyeonekana akienda mbele lakini akili yake shingo yake ikigeuka kama bundi akimtazama Joy kwa jinsi alivyoacha nusu na robo ya umbile lake nje.
“Ni mteja mwenye aibu mfuate,” ni sauti iliyokuwa ikizungumza ndani ya Joy, akaitii na kumfuata yule mtu, “kaka twende nikakupe raha,” alisema Joy bila ya aibu;
“Shingi ngapi?” aliuliza yule kaka aliyeonekana mzoefu ila mdhambi wa sirisiri maana aliongea akiwa gizani kweli.
“Elfu 10 kwa showtime, elfu 30 hadi asubuhi na unanishika kokote unapopenda,” alijibu Joy macho yake yakiwa makavu kweli.
“Poa, twende,” alizungumza yule jamaa , Joy akamuongoza kuelekea kwenye ile gesti yake ambayo muda mchache uliopita alikuwa amenusurika kesi ya mauaji.
Nini kitafuatia Itaendelea kesho wala hautakiwi kukosa
Chanzo. Fred njeje
No comments:
Post a Comment