Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la wazee wa Yanga wamesema wanamuunga mkono Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Yusuph Manji kuelekea uchaguzi mkuu wao unaotarajiwa kufanyika Juni 25 mwaka huu kufuatia kukaa miaka miwili nje ya katiba bila kuwa na kiongozi wa juu.
Akizungumza huku wakionesha msimamo wao kama baraza la wazee la Yanga wakiwa kwa pamoja na wenyeviti wa matawi wa mkoa wa Dar es salaam, Katibu wa baraza hilo Ibrahim Akilimali amesema kuwa wanamuunga mkono Manji kwa asilimia zote kwani ameweza kuisaidia timu hiyo toka akiwa mdhamini mpaka kufikia kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Kwa upande wa baraza la wazee tunamuunga mkono Manji kwani toka Yanga imekuwa chini yake kumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuweza kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho na kama kuna masuala mengine ikiwemo ya uwanja uongozi mpya utakapoingia tutakaa nao kuweza kujua tunafikia wapi malengo yetu ya kujenga kwani tumeshafikia kwenye hatua bado kibali tu,"amesema Akilimali.
Amesema, watu wasitake kuangalia suala la Uwanja kwa Manji tu mbona kuna viongozi wengine wamepita na hawajajenga cha msingi ni kuangalia wapi tunaelekea na nini kinachotakiwa kufanyika kwenye klabu kwa ajili ya maendeleo.
Wazee hao wamesema kwa pamoja kuwa mbali na hilo pia wanawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 26 pamoja na kuingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirishiko ikiwa ni moja mafanikio wanayojivunia chini ya Manji.
No comments:
Post a Comment