“Unabisha nije?”
“Sibishi bwana, usije ukaja kweli ikawa noma.”
“Mi hamnazo unajua.”
JIACHIE MWENYEWE
Aisha alijiambia moyoni kwamba hatakwenda kulala hadi ashikwe na usingizi sana ili akifika kitandani iwe ni kujitupa tu, puu! Mpaka kunakucha! Hataki kushikwa wala kupapaswa…
“Akirogwa kutaka kunishika ole wake, nitamtukana mpaka akome,” alisema moyoni Aisha huku akianza kusinzia kwa mbali.
***
Ilikuwa saa kumi na moja alfajiri, Beka alishtuka kutoka usingizini na kukuta mkewe amelala eneo lake. Alitoka kitandani akiwa ndani ya bukta na kufungua mlango, akatoka sebuleni.
Alikaa kwa muda, alipotupia macho saa ya ukutani na kubaini ni saa kumi na moja na dakika kumi na tano, alisimama, akatembea hadi kwenye chumba alicholala shemeji yake, alisukuma mlango akabaini ulifungwa kwa ndani.
Beka aligonga kwa mbali huku akihisi kibaridi ambacho kilimpiga mwilini hivyo kuhitaji sana joto la mwanamke na mwanamke mwenyewe si mke wake kwani alijua mkewe angemkatalia tu.
Dada wa Aisha kwa sababu alishaamka usingizini, kilichokuwa kimebaki ni kutoka kitandani tu, aliweza kusikia mlango ukigongwa kwa mbali, akashtuka…
“He! Atakuwa nani huyo?” alijiuliza.
Alitoka kitandani, akataka kuuliza kwa sauti we nani lakini akili ilimwambia anaweza kuwa mume wa mdogo wake, kwa hiyo kama atauliza atasikika.
Alifungua mlango, akasimama akiwa nusu ndani, nusu nje…
“Vipi shemeji?” aliuliza dada mtu huyo kwa sauti ya chini.
Kwa Beka sauti hiyo ilikuwa tamu sana kwani aliamini kwamba kitendo cha kujibiwa kwa sauti ya chini ni ishara ya kukubaliana na faragha…
“Poa vipi, umeshaamka?” aliuliza Beka swali lenye jibu hata kabla hajajibiwa…
“Nimeamka ndiyo,” alikubali dada mtu huku moyoni akisema…
“Ningekuwa sijaamka ningekuja kufungua mlango? Na wewe shemeji bwana maswali yako.”
“Vipi, naweza kuingia?”
“Ha! Uingie halafu akijua?”
“Amelala na yule ninavyomjua kuamka kwake saa mbili asubuhi.”
“Mh! Shemeji lakini wewe, huogopi kabisa?” dada mtu alihoji lakini huku na yeye akipigwa na kibaridi ambacho alijua kingetoka kwa njia ya kushikwashikwa na mwanaume kama Beka achilia mbali mume wake.
Alijikuta akiuachia mlango ili Beka apite, akapita hadi chumbani na kukaa kitandani. Dada mtu huyo alikuwa akitetemeka mwili lakini pia alisisimkwa kwani uhitaji wa mahaba ulipanda kwa kiwango cha juu kwa wakati huo.
“Sasa shemu tusipoteze muda bwana,” alisema Beka huku akivua bukta yake na kuitupa chini.
Dada mtu alipolala alikuwa amejifunga kanga moja tu kwa hiyo hakuwa na sababu ya kujichojoa sana, aliifungua kwenye upindo mmoja na kuitupia kanga juu ya kitanda.
Beka alipanda kitandani, dada mtu naye alishapanda. Wote walikuwa juu ya kitanda, Beka alipeleka mkono kwa mara ya kwanza kwenye mwili wa dada mtu, akaungwa mkono.
Kwa sababu ya kuiba, haraka ilikuwa inatakiwa hivyo hawakuchelewa, wakaingia uwanjani. Ni kweli kila mmoja alikuwa na siku nyingi za uhaba wa mapenzi kwa hiyo walipoanza mechi tu, msisimko ulikuwa mkubwa sana, ilikuwa ni uwezo wa kipekee kwa dada mtu kujizuia asipige kelele kwani vigezo vyote vya kufanya hivyo alikuwa navyo.
Hata wakati dada mtu huyo anafika juu ya kilele cha mlima waliokuwa wakiupanda, Beka alijua kwa jinsi alivyong’ang’aniwa kwa kubanwa kwa nguvu zote.
Hata yeye Beka alipokuwa anafika kwenye ncha ya kilele hicho, alimbana sana dada mtu hivyo naye akawa amewakilisha tukio bila maneno wala sauti.
Hakuwa na sababu ya kuendelea kufanya shoo juu ya kitanda hicho kwani wote walijiridhisha, sasa nini tena walikuwa wakikitaka? Maana kama ni fumanizi halikutokea! Beka alitoka kitandani, akavaa bukta na kutimua zake kurudi chumbani.
Jua lilitoka, Aisha aliamka na kutoka kabisa chumbani. Alikwenda nje na kukutana na dada yake…
“Shikamoo dada.”
“Marahaba, umeamkaje mdogo wangu?” aliitikia dada mtu huku akikimbiza uso pembeni ili wasionane kwa usaliti alioufanya na mume wake usiku uliopita.
“
Nimeamka poa tu. Dada nisamehe sana kwa jana usiku, si nia yangu dada angu. Unajua nilikasirika kwa sababu ni kweli shemeji yako hajawahi kunisifia hata siku moja na mimi kama mimi najisikia vibaya sana.”
“Mimi mbona nimekuelewa mdogo wangu wala usijali. Atajirekebisha tu.”
Pitapita ziliendelea, sasa ikawa dada mtu akimwangalia mdogo wake anajisikia aibu lakini moyoni anajipongeza kwa kitendo cha kukata kiu na shemeji yake…
“Lakini kama ni kosa analo mwenyewe Aisha, yeye kumnyima unyumba mume wake anatarajia nini hasa, yule ni mwanaume, ana matamanio kama binadamu. Ni upuuzi wa hali ya juu, mumeo kabisa eti unamkatalia tendo la ndoa.”
***
Usiku wa siku hiyo wakati wa mlo wa usiku, watatu hao walikuwa wamekaa kwenye meza ndani ya chumba cha chakula.
Beka hakuwa msemaji sana, ni kama shemeji yake tu, naye hakuwa msemaji kama siku nyingine. Hali hiyo ilimshangaza sana Aisha kwani kwa anavyojua yeye, mumewe ana mathulubu sana kwa dada yake. Mara amwite mke, mara asimfie, mara amponde kuhusu kuachika kwa mume wake, ilimradi.
Kumbe wakati Aisha akijiuliza hivyo, wenzake miguu chini ya meza ilikiwa ikiwasiliana ile mbaya. Miguu ya dada mtu ilipanda hadi karibu na magoti ya Beka naye akarudishia. Ilikuwa kama wanacheza, kama Aisha angeona mioyo ya wawili hao angegundua ni jinsi gani walivyokuwa na amani ya kitendo chao hicho cha kupandishiana miguu.
Ilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua, Aisha aliinamisha kichwa na kuchungulia chini kama mtu aliyeona kitu kisichokuwa cha kawaida.
Inaendelea
Chanzo globalpublishers
No comments:
Post a Comment