Social Icons

Siasa



ZIARA YA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI ALHAJI ABDALLA BULEMBO MKOANI MBEYA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo alifanya ziara katika mkoa wa Mbeya ,na kutembelea wilaya zote za mkoa wa Mbeya. Chini ni picha za majumuisho ya ziara hiyo pamoja na mkutano wa hadhara alioufanya katika kata ya Nzovwe katika jiji la Mbeya.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akisalimiana na viongozi wa CCM alipowasili makao makuu ya CCM Mkoa wa Mbeya.

Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimkalibisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya.

Mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe. Rosemary Senyamule na  Mbunge wa Ileje Mhe. Aliko Kibona wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mikutano.


   Mwenyekiti wa Wazazi akiwasili katika uwanja wa Nzovwe tayari kwa mkutano wa hadhara.




Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Mhe. Zambi akimkaribisha Mwenyekiti wa Wazazi katika uwanja wa Nzovwe.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia umati wa watu waliohudhuria mkutano wake katika uwanja wa Nzovwe.


    Mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe. Rosemary Senyamule akiwasalimia wananchi wa Nzovwe.


Vijana waendesha boda boda wa Nzovwe wakiwa na furaha baada ya kupwewa kadi za CCM na kuachana rasmi na CHADEMA.

Maelfu ya vijana wa jiji la Mbeya wakishangilia mkutano wa CCM katika uwanja wa Nzovwe.



Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mbeya mama Fatuma Kasenga akiwasalimia wananchi waliofurika katika uwanja wa Nzovwe.

Meya wa jiji la Mbeya na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbaraliwakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa            Wazazi Taifa

   Siku hiyo ilikuwa ni furaha kwa kila mwanaCCM kama wanavyoonekana akina dada hawa.


                 Vijana nao hawakuwa nyuma katika kufurahia mkutano huo wa CCM.


                                                     Picha zote na Bashiru Madodi

No comments:

 
 
Blogger Templates