Social Icons

Thursday, 22 August 2013

HATI ZA KUMILIKI ARDHI ZITOLEWE UPYA, ZA DIJITALI NA ZIWE NA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)- Zitto Kabwe

Kamati ya Hesabu za Serikali imekutana na Wizara ya Ardhi kwa madhumuni ya kupitia Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2012. Changamoto za Wizara ni nyingi sana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amehoji mambo mengi sana na mengi ni wizi, upotevu wa mapato ya Serikali na malalamiko ya wananchi kuhusu ardhi. CAG alitoa hoja za ukaguzi maeneo ya mapato kutokusanywa, kulimbikizwa na hata kukusanywa bila kuyawasilisha Wizarani.

Katika Mwaka wa Fedha 2011/12 Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni tisini na tisa (99 bilioni) lakini ilikusanya shilingi bilioni ishirini tu (20 bilioni) sawa na asilimia 21 ya makadirio.

CAG pia alihoji masuala ya viwanja vilivyopimwa, kugawiwa watu lakini watu hawakupewa hati ambapo zaidi ya viwanja 7, 342 vilikutwa ni viwanja vyenye shaka. Pia viwanja 160 jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 555.8 milioni viligundulika ni viwanja ambavyo walijigawiwa maafisa wa Ardhi maana haoakuwa na ushahidi wowote wa mauzo ya viwanja hivyo. Hoja nyingine ni pamoja na ukiukaji wa sheria kwa kujengwa kwenye fukwe nk.


No comments:

 
 
Blogger Templates