Katika mchezo huo timu ya watoto wa mjini Bagamoyo Stars iliibugiza timu ya Juhudi magoli 2-1, mpaka timu hizo zilipokuwa zinakwenda mapumzikoni timu ya Bagamoyo Stars ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0, kipindi cha pili kilipoanza vijana wa mjini Bagamoyo Stars haikuwachelewesha Juhudi Stars kwani walipachika goli la pili dakika za mwanzo tu za kipindi hicho.
Baada ya kufungwa goli la pili vijana wa Juhudi walikuja juu na kulishambulia lango la Bagamoyo, katika mashambulizi hayo mabeki wa Bagamoyo walijichanganya na beki wa kati kujikuta ameunawa mpira katika eneo la hatari, hivyo kuipatia penati timu ya Juhudi Stars.
Penati hiyo ilipigwa kifundi na mchezaji wa Juhudi na kuipatia timu hiyo goli la kufutia machozi, hivyo mpaka refa wa mchezo huo Mbwana anapuliza kipenga cha kumaliza mchezo huo Bagamoyo stars ilitoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1.
Mashabiki wa Bagamoyo Stars wakishangilia ushindi baada ya mchezo kumalizika na timu
Yao kuibuka na ushindi wa goli 2-1
Kikosi cha timu ya Bagamoyo Stars
Mashabiki wa Bagamoyo Stars wakipuliza Mavuvuzela wakati wa mchezo ili kuwapa moyo
wachezaji wao.
Picha zote na Bashiru Madodi
Ijumaa 16, Agosti, 2013: www.basahama.blogspot.com
2 comments:
Hongera Bagamoyo Stars! Ila mimi,kama mzawa wa Bagamoyo, bado siko nanyi kwenye jina, na sasa nimegundua hata bendera, SIONI SABABU YA MANENO MAWILI, Stars na Washington DC! BADALA YAKE, Iwe Bagamoyo Sports Club! Rungwe .......!
Naomba kupata MAJINA ya kikosi kizima cha timu pamoja na uongozi wake!
Post a Comment