TUESDAY, AUGUST 27, 2013
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. MUHONGO AKAGUA MAENDELEO YA UTANDAZAJI MABOMBA YA GESI MTWARA-DAR
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
No comments:
Post a Comment