Katibu wa Itikadi na Uenezi -CCM Nape Nnauye
---
UTEUZI
Kikao cha Halmashauri Kuu pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.
Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.
Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).
Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.
Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.
Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC
- Ndugu Ashura Amanzi
- Ndugu Rukia Saidi Mkindu
- Ndugu Elias J. Mpanda
- Ndugu Jonathan M. Mabihya
- Ndugu Mulla Othman Zuberi
- Ndugu Jumanne Kapinga
- Ndugu Ali Haji Makame
- Ndugu Jacob G. Makune
- Ndugu Juma A. Mpeli
- Ndugu Hawa Nanganjau
- Ndugu Abdulrahman Shake
- Ndugu Subira Mohamed Ameir
- Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
- Ndugu Juma Bakari Nachembe
- Ndugu Josephat Ndulango
- Ndugu Rajab Uhonde
- Ndugu Abeid Maila
- Ndugu Mohamed Lawa
- Ndugu Mariam Sangito Kaaya
- Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
- Ndugu Julius Peter
- Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
- Ndugu Mathias Nyombi
- Ndugu Mohamed Hassan Moyo
Chanzo:- Dodoma yetu
No comments:
Post a Comment