Akiwasili viwanja vya Gymkana ambavyo vipo jirani kabisa na mahakama hiyo
Baadhi ya wananchi waliofurika kwenye mahakma hiyo
Polisi wakikagua helkopta hiyo baada ya Ponda kushuka
Helkopta hiyo ikiruka kumrejesha Ponda gerezani jijini Dar es salaam.
NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO-
Katibu wa taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda mkazi wa Dar es salaam leo asubuhi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro kwa usafiri wa helkopta ya jeshi la polisi kujibu shitaka linalomkabili.
Ponda alifikishwa mahakamni hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wakiwa na mbwa baada ya kuwasili kwa herikopta hiyo iliyotua majira ya saa tatu subuhi katika uwanja wa Gofu mjini Morogoro ikitokea jijini Dar es salaam.
Wakili wa Serikali,Bernard Kongola alikisoma mashitaka matatu dhidi ya Shekhe Ponda mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate alisema, mnamo Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro Ponda aliuambia umati wa watu uliokusanyika kwenye mkutano wa hadhaza “ndugu waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bwakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na watajitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti,fungeni milango na madirisha ya msikiti yenu na muwapige sana”
Kongola aliimbia mahakama hiyo kuwa kauli hiyo iliumiza imani za watu wengine na kwamba hatua hiyo ni kinyume cha agizo la mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar-es-salaam iliyotolewa na hakimu V. Nongwa mei 9 mwaka huu ambayo ilimtaka Ponda ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja kutohubiri mambo ya uchochezi ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 124 cha mwaka 2002, shitaka ambalo alikana.
Chanzo:- michuzijr.blogspot.
No comments:
Post a Comment