Pia alielezea umuhimu wa wajumbe kujua kuwa nafasi yao ni kubwa na dhamana yao ni kubwa, kwani zoezi kama hili siku za nyuma lilikuwa linafanywa na Bunge, lakini leo limeletwa kwa wananchi kwa kupitia uwakilishi wa wajumbe mliomo katika ukumbi huu, alisema Profesa Baregu.
Pia Profesa Baregu aliwakumbusha wajumbe umuhimu wa maoni yao kwani kila mjumbe aliye katika ukumbi huu anawakilisha Watanzania zaidi ya 2000. Kwa hiyo matumaini ya wananchi na taifa yako mikononi mwa wajumbe mliochaguliwa na wenzenu katika kata zenu.
Kiongozi wa tume Profesa Mwesiga Baregu akifungua mkutano Baraza la kujadili Rasimu ya Katiba
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Wajumbe wa Baraza la kujadili Rasimu ya Katiba wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Wakimsikiliza Profesa Baregu.
Kiongozi wa Tume ya mabadiliko ya katiba akitoa maelekezo ya namna mjadala wa Rasimu
ya Katiba utakavyondeshwa.
Picha zote na
Bashiru Madodi.
No comments:
Post a Comment