Uenezi neno linalotumika sambamba na propaganda, likiwa na maana ya matumizi ya njia za mawasiliano zenye madhumuni ya kuteka hisia na fikra za watu kuelekea kwenye lengo maalumu.
Neno propaganda lilipewa uzito na kutumika kama dhana kutokana na matumizi yake ya kimsimamo na mwelekeo katika medani za vita, mabadiliko ya dini (Reformation) na hatimae katika siasa kama tutakavyoona.
HISTORIA YA PROPAGANDA
Propaganda ilianza kutumika na kuwekwa rasmi kama vitendo vya binadamu katika vita ya mwaka 515 BC (kabla ya kuzaliwa Kristo) katika vita ya PERSIA ya wakati ule. Aidha propaganda ilitumika India kunako mwaka 350 mpaka 383 BC, vile vile katika matumizi ya vita.
Maandishi ya propaganda za Kirumi yalionekana kati ya mwaka 59 BC na 17 AD. Warumi ndio waliolipa jina propaganda kuwa PROPAGALE katika Kilatini, likiwa na maana ya kueneza. Ni tafsiri ya jina hilo ambalo linatumika mpaka sasa.
Kule Soviet union wakati ule propaganda ilitumika katika kueneza fikra za kimapinduzi, mafundisho ya elimu ya uchumi wa Marxist (Marxist Economy), na kushawishi maoni ya umma na kuwafanya wajiunge katika vugu vugu au harakati za kisiasa. Kazi hiyo iliungwa mkono na Stalin. Yeye alitumia ndege kubwa katika kupeperusha vipeperushi vya agitation (uchochezi).
Tangu wakati ule, wana-nadharia wamekuwa wakitumia propaganda na agitation katika medani, wakati, na malengo tofauti.
Tangu wakati ule, wana-nadharia wamekuwa wakitumia propaganda na agitation katika medani, wakati, na malengo tofauti.
UHUSIANO KATI YA PROPAGANDA NA AGITATION
Kama ilivyoelezwa katika ainisho lake, propaganda ni kuteka hisia na fikra za watu kuelekea kwenye lengo maalumu. Watu wenye kufanya shughuli hizo huitwa Propagandists. Katika medani za siasa Propagandists huwa ni kiongozi au makada wa chama walioandaliwa na wenye kuelewa vizuri itikadi na sera za chama.
Hawa wanategemewa kuwa wasemaji wazuri, wanajua kujenga hoja kuhusu kueleza, kufafanua, kutetea na kulinda itikadi na sera za chama. Aidha wanatakiwa kujibu uongo na hadaa za wapinzani wao wa kisiasa kwa nguvu za hoja. Propagandists wazuri hufanya utafiti wa kina kuhusu mambo wanayotaka kuyatumia katika propaganda.
Na wanatakiwa kujua wakati muafaka wa kufanya propaganda ama kwa kufanya uenezi au agitation kwa kujibu mapigo ya wapinzani.
Kwa upande mwingine wapo Political Agitators ambao vile vile huitwa ACTIVISTS au MILLITANTS. hawa hufanya kazi ya siasa ya mtu kwa mtu au makundi madogo madogo ya watu. Wao huanzia na hoja maalumu "SPECIFIC" iliyo ndogo na kisha kuipanua na kufikia lengo kwa ujumla wake. Kama ni kujibu hoja activists hujibu hoja papo kwa papo na huwa hahitaji maandalizi makubwa.
MATUMIZI MABAYA YA PROPAGANDA
Propaganda ilichukua sura mpya wakati wa Adolf Hitler alipochukua madaraka ya Ujerumani mwaka 1933. Yeye aliamini kuwa Propaganda ni chombo muhimu katika kutimiza malengo yake.
Aliunda wizara maalumu na kumteua Joseph Goebbel kuwa kiongozi wake. Yeye aliwaamuru waandishi wote wa habari na radio ili watumike katika Propaganda. Ni wakati huo ndipo tulipoona matumizi mabaya ya Propaganda, katika kanuni iliyoitwa.
Aliunda wizara maalumu na kumteua Joseph Goebbel kuwa kiongozi wake. Yeye aliwaamuru waandishi wote wa habari na radio ili watumike katika Propaganda. Ni wakati huo ndipo tulipoona matumizi mabaya ya Propaganda, katika kanuni iliyoitwa.
GOEBBELS PRINCIPALE.
Kanuni hiyo ilianzishwa na Goebbels kwa kuandaa mikakati ya kutangaza uongo na upotoshaji dhidi ya adui na kuurudia mara nyingi kadili ilivyowezekana mpaka Wajerumani walifika mahali wakakubali na kuamini uongo au upotoshaji uliokuwa unatangazwa.
Hapo ndipo ilipoanzishwa kanuni ya Goebbel inayosema " Uongo ukirudiwa mara nyingi bila ya kukanushwa unakuwa ukweli"
Kanuni hii ya Goebbel iliipa propaganda maana mbaya kwa kupotosha maana na matumizi yake yaliyokuwa yamezoewa na watu wengi.
Hapo ndipo ilipoanzishwa kanuni ya Goebbel inayosema " Uongo ukirudiwa mara nyingi bila ya kukanushwa unakuwa ukweli"
Kanuni hii ya Goebbel iliipa propaganda maana mbaya kwa kupotosha maana na matumizi yake yaliyokuwa yamezoewa na watu wengi.
VIPENGELE VYA PROPAGANDA
Vipengele vya propaganda vinajikita katika kuteka hisia na fikra za watu kwa ajili ya kufikia lengo maalumu, kwa kutumia njia ya mawasiliano. Hapa kuna umuhimu kwa wana propaganda kufahamu hisia za watu wanazoweza kuzitumia. Hisia hizo ni:-
1. UPENDO: Kumfanya mtu apende kile kitu ambacho wewe unataka akipende.
2. MATUMAINI: Kumpa mtu matumaini kuhusu jambo fulani linalomuhusu au Kumgusa kwa njia moja au nyingine.
3. CHUKI: Kumfanya mtu achukie kitu au jambo unalotaka achukie.
4. HOFU: Kumtia mtu hofu kuhusu jambo ambalo wewe unataka awe na hofu nalo.
Kwa leo tushie hapa katika siku za mbele katika makala yangu nitafafanua zaidi kuhusu
propanganda na aina za propaganda.
Imetayarishwa na
Bashiru Madodi.
Ijumaa, 16, Agosti, 2013. www.basahama.blogspot.com
No comments:
Post a Comment