Dk. Lu, alisema nchi yake imejipanga kujenga viwanda vya kisasa katika Mkoa wa Shinyanga, ambavyo vitatoa ajira kwa vijana na kwamba hiyo ni kutokana na uhusiano mzuri iliyonao na CCM.
Akizungumza katika mikutano iliyofanyika juzi na jana katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga Mjini, Dk. Lu, alisema pamoja na Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi, anaamini kuwa CCM bado iko imara na inaweza kuendelea kuongoza kwa muda mrefu.
“Kwa hili inadhihirisha kuwa hakuna chama kama CCM kutokana na uimara wake na hili wanalofanya sasa la kuja kuimarisha chama nasi kule China kupitia chama chetu tawala cha CPC, tunafanya kama hivi pia. Mwadilaaaaa Shinyanga, CCM oyeeeeee asante sana,” alisema.
Balozi huyo ambaye muda mwingi alikuwa ameandamana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, alisema nchi yake imejiandaa vizuri katika sekta ya uwekezaji.
China na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri ambao umekuwapo tangu uongozi wa Rais Julius Nyerere na Rais wa China wakati huo, Mao Tse Tung.
Chanzo:- Mwananchi.
No comments:
Post a Comment