Ili kukabiliana na makundi hayo, alisema chama hicho kimeweka utaratibu wa kutotoa kadi za uanachama kwa wanachama wapya katika kipindi cha miezi sita kabla ya uchaguzi.
Kinana alitoa kauli hiyo jana wilayani Maswa, Mkoa wa Mwanza, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo.
Kinana, ambaye yupo katika ziara ya kuimarisha chama katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akiwa ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema hakuna mjadala katika usimamizi wa agizo hilo.
Alisema hivi sasa kuna watu katika ngazi za mikoa na wilaya, wamekaa mahali wakiwa na kazi ya kuwaandaa wana CCM pamoja na kuwanunua ili wapate nafasi za uongozi serikalini.
“Ninachotaka kusema ni kuwa, chama kitaheshimu maamuzi ya wanachama, lakini siyo ya wale ambao wamekaa sehemu kwa lengo la kushawishi watu ili wachaguliwe wao huku wakishindwa kuheshimu utaratibu wa chama.
“Kama wewe unajiona ni kiongozi unafaa, basi tambua wenye jukumu la mwisho ni wana CCM na sio utashi wako wa fedha au ubabe katika kutaka nafasi ya uongozi.
“Kwa sasa CCM iko macho, kwani imepata funzo kutokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo baadhi ya watu waliochaguliwa walitoa rushwa huku wenye sifa wakiachwa kutokana na kukosa fedha,” alisema Kinana.
Alisema katika kusimamia uadilifu, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula, hawako tayari kuyumbishwa na watu ambao wana lengo la kutaka kuvuruga umoja na mshikamano ndani ya CCM.
Alisema kwamba, kama kila kiongozi pamoja na wanachama watashikamana kwa ngazi zote, mwaka 2015 ushindi utapatikana, ikiwa ni pamoja na kukomboa majimbo ya uchaguzi yanayoongozwa na vyama vya upinzani.
“Ukifika wakati wa uchaguzi tumeweka sheria na utaratibu wetu, ikiwemo kufunga leja za wanachama miezi sita kabla ya uchaguzi.
“Kama kuna kiongozi, hasa Katibu wa ngazi yoyote, ile atakwenda kinyume na agizo hili, hatua kali za kisheria za kichama zitachukuliwa dhidi yake.
“Kila wakati nasema kwamba kinacholeta matatizo katika uchaguzi ni fedha, kwani baadhi ya watu wanaufanya uchaguzi kuwa kama mradi wao wa kupata fedha, tambueni wanaofanya vitendo hivi wanafanya makosa makubwa,” alionya Kinana.
Chanzo:- Mtanzania.
No comments:
Post a Comment