Social Icons

Friday, 13 September 2013

DIWANI WA KATA YA KIWIRA AFUMANIWA NA MWANAFUNZI....

Diwani wa Kata ya Kiwira Wilayani Rungwe, Lawland Mwakalibule leo amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi anayesoma katika Shule ya Sekondari Kiwira, kidato cha Tatu. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Binti huyo alitoweka nyumbani kwao tokea jana, mpaka alipolejea leo asubuhi, wazazi wake walipombana awaeleze wapi alilala usiku wa leo ndipo aliposema kuwa alilala na Mhe. Diwani Lawland Mwakalibule.

Baada ya kupata maelezo hayo wazazi wa mwanafunzi huyu walichukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira. Polisi walichukua hatua ya kumtafuta diwani Mwakalibule na kumuweka chini ya ulinzi wakati upelelezi wa tukio hili ukiendelea. Mtuhumiwa kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Rungwe mjini Tukuyu.

Mpaka mwandishi wetu anatoka katika kituo cha polisi mjini Tukuyu mtoto wa shule alikuwa amepelekwa hospitali ya Wilaya ya Rungwe 'Makandana' kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Kituo cha Polisi Tukuyu mahali ambako Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wa shule ya Sekondari Kiwira.

Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule akiwa chini ya ulinzi wa Polisi katika kituo kikuu cha Polisi mjini Tukuyu.

                                              Picha zote na Basahama blog.



No comments:

 
 
Blogger Templates