Social Icons

Wednesday 11 September 2013

KIKAO CHA BARAZA MAALUMU LA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE..



* Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. 2011-2012

* Kikao kilikuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.

Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo imekutana katika kikao maalumu cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa mwaka 2011-2012. Kikao ambacho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro akiwasili makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, kwa ajili ya kikao cha Baraza Maalumu la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula akifungua kikao cha Baraza Maalumu la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Na kumkaribisha mkuu wa mkoa  wa Mbeya kwa kumwambia kuwa wako tayari kwa ushauri na maelekezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro akitoa maelezo ya awali ya kuashiria kuanza kwa kikao cha Baraza Maalumu. Na kuwakumbusha wakuu wa idara kuacha ubabaishaji katika kazi zao.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali toka tawi la Mbeya Ndugu, Baraka Mahenge akikiongoza kikao kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2011-2012.

Wakaguzi kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Tawi la Mbeya Ndugu, Baraka Mahenge na Ndugu, Athumani Mohamed, wakikisimamia kikao

Wakuu wa Idara wakiwa wamesimamishwa na Mkuu wa Mkoa ili kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakiwa katika kikao cha Baraza Maalumu la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

                         Wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

             Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro akisisitiza jambo wakati wa kikao

Mkuu wa Mkoa Mhe. Abbas Kandoro akiendelea kutoa msisitizo kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Kuhusiana na hoja zilizokuwa mbele yao. Na kuwasisitiza kuwa suala la kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali si jukumu la Mtunza Hazina wa Wilaya peke yake bali ni suala timu nzima ya Halmashauri likishirikisha Madiwani katika kamati zao na kwenye kata zao na pia watendaji katika idara zao wanazoziongoza kwa kuwa wao ndiyo watumiaji wa fedha.

Mkuu wa mkoa akihitimisha kikao baada ya kumaliza kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi  wa hesabu za Serikali CAG, alisisitia hoja kutokujirudia mala kwa mala, pia aliwataka watendaji na watoa maamuzi kufanya maamuzi ya haraka ili fedha zinazoletwa katika Halmashauri zitumike kwa wakati na bila kubaki wakati wa mwisho wa mwaka, pia alisisitiza Kamati ya ukaguzi ifanye kazi zake na ikutane kwa 
mujibu wa sheria. 

Mkuu wa Mkoa aliendelea kusisitiza Halmashauri kuwa na mikakati ya kujitegemea, kwa kuangalia jinsi ya kuwawezesha wakulima, wafugaji, na wajasiliamali. tusimamie viwanda vyetu vidogo vidogo. Pia aliutaka uongozi wa Halmashauri kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa hawana madai kwa sababu ya watendaji wa Halmashauri kutokuwajibika, na kusababisha madeni yasiyo na ulazima kwa Halmashauri.

chanzo:- Basahama Blog.

















1 comment:

Anonymous said...

Ndugu Madodi

Asante sana kwa taarifa zako nzuri. You are really up to date. Be blessed. Mwambalaswa - Kyela

 
 
Blogger Templates