Kamati ya Fedha Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo imeendelea na ukaguzi wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo. Miradi iliyokaguliwa leo ni ifuatayo, Ujenzi wa nyumba za Watumishi Zahanati ya Igalamu, Ujenzi wa matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi Itiki, Ujenzi wa Kiwanda cha Matunda Iponjola, Ujenzi wa Kituo cha Rasilimali cha Wakulima Ilenge Ujenzi wa Jengo la Utawala Ilenge, na Ujenzi wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Lupoto.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota wa kwanza kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Igalamu kuhusiana na ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa Zahanati ya Igalamu iliyopo katika Kata ya Malindo Wilayani Rungwe.
Picha juu ni majengo mawili ya nyumba za watumishi wa Zahanati ya Igalamu, nyumba hizo zikikamilika zitaghalimu Shilingi Milioni 62, Fedha zote zimetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Choo cha zamani kilichopo katika Shule ya Msingi Itiki iliyopo katika Kata ya Lufingo
Choo kipya kinachojengwa katika Shule ya Msingi Itiki kwa gharama ya Shilingi Milioni 2,400,000/= katika Kata ya Lufingo Wilayani Rungwe.
Jengo la Kiwanda cha Matunda Iponjola kama linavyoonekana wakati wa ukaguzi, jengo hili mpaka likikamilika litagharimu Shilingi Milioni 46,
Jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kyimo iliyopo katika kata ya Kyimo, jengo hili lilipewa Shilingi Milioni 7 na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya Umaliziaji wa Jengo hili.
Jengo la Kituo cha Rasilimali cha Wakulima Ilenge, jengo hili lilitengewa Shilingi Milioni 15, na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya gril na kupiga plaster ndani ya jengo. Kazi ambayo tayari imefanyika.
Sehemu ya jengo la Maabala linalojengwa katika Shule ya Sekondari Lupoto iliyoko katika kata ya Ibigi
Sehemu ya ujenzi unaoendelea wa ujenzi wa madarasa matatu yanayojengwa katika Shule ya Sekondari Lupoto iliyoko katika Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe.
Sehemu ya matundu ya vyoo 7, kati ya 14 yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Lupoto
Msingi wa nyumba ya mwalimu inayojengwa katika shule ya Sekondari Lupoto.
Mradi wa ujenzi wa madarasa matatu, ukarabati wa madarasa matatu, matundu ya vyoo 14 na maabala moja unaotekelezwa katika shule ya Sekondari Lupoto, picha juu zinaonyesha maendeleo ya mradi huu unavyoendelea
Picha na Bashiru Madodi
Basahama blogspot
No comments:
Post a Comment