Social Icons

Monday, 16 September 2013

UKAGUZI WA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE

Kamati ya Fedha Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo imetembelea miradi minne kwa ajili ya ukaguzi miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa Shule ya Msingi Nzunda, Matengenezo ya sehemu korofi barabara ya Idweli - Ngumbulu Km 3, Ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Ngumbulu na Ujenzi wa daraja la Malangali kata ya Swaya.

Picha chini ni ukaguzi na maeneo yaliyokuwa yanakaguliwa pamoja na gharama za mradi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mhe. Alfred Mwakasangula akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota wakati wa ukaguzi wa miradi

L
Jengo la Shule ya Msingi Nzunda iliyo katika Kijiji cha Ntokela kata ya Isongole, Shule hii imejengwa na wananchi wa Kijiji cha Ntokela. Wananchi hao wamejenga shule, nyumba ya mwalimu pamoja na matundu sita ya vyoo kwa gharama ya Shilingi Milioni 55.

Barabara ya Idweli - Ngumbulu ikiendelea kutengenezwa na kampuni ya Ikimbu Company Ltd kama inavyoonekana wakati wa ukaguzi wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango. Barabara hii ya Km 3 inajengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 98. Mpaka itakapokuwa imekamilika.

Nyumba ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Ngumbulu ikiwa katika hatua za umaliziaji nyumba hii mpaka itakapo kamilika itagharimu shilingi Milioni 14, hii ni pamoja na nguvu za wananchi shilingi 645,000/- fedha zingine zimetolewa na LGCDG.


Daraja la Malangali katika kata ya Swaya likiwa limekamilika na tayari kwa matumizi, daraja hili limejengwa kwa fedha za Road Fund kwa gharama ya Shilingi Milioni 30.

                                                     Picha zote na Basahama Blog





No comments:

 
 
Blogger Templates