Social Icons

Sunday, 15 September 2013

WAZIRI WA JAKAYA KIKWETE ANAPOPAGAWA NA MECHI YA YANGA NA MBEYA CITY...

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philip Mulugo jana alikuwa ni burudani tosha katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, baada ya kuwaongoza mashabiki wa soka jijini Mbeya kuishangilia timu ya Mbeya City dhidi ya Yanga. Mhe. Mulugo alikuwa katikati ya mashabiki na kuwaimbisha CCM, CCM, CCM. kila wakati timu ya Mbeya City ilipokuwa inafanya mashambulizi katika goli la Yanga.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philip Mulugo akiongea na waandishi wa habari baada ya mechi kati ya Yanga na Mbeya City.

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Mulugo akielezea furaha yake kwa waandishi wa habari jinsi vijana wa Mbeya City walivyomfurahisha kwa mchezo safi na wa uhakika.

Mhe Mulugu akitoa kauri kuhusu ahadi yake kwa Mbeya City ikiifunga Yanga kuwapa shilingi Milioni mbili, Mhe. Mulugu alisema kwa kuwa wametoka suluhu basi anawapatia Mbeya City milioni moja ambayo aliitoa hapo hapo uwanjani sokoine.



Picha hizo tatu Mhe. Philip Mulugo akiwa katikati ya mashabiki wa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, akiongoza hamasa dhidi ya Yanga.

Hali ya usalama ilivyokuwa wakati wa mchezo kati ya Yanga na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

                                                    Picha zote na Basahama blog.





No comments:

 
 
Blogger Templates