Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa akiongea kwenye kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na wasomi wa Vyuo Vikuu vilivyoko Mkoani Mbeya.
Dr. Mary Mwanjelwa akiendelea kuwapa nasaha vijana katika ukumbi wa Mtenda
Dr. Mary Mwanjelwa akikabidhi kadi kwa wananchama wapya wa UVCCM
Wanachama wapya wa UVCCM wakila kiapo cha uaminifu
Vijana wa UVCCM mjini Mbeya
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, amesema baadhi ya wanachama wa chama hicho wanakiangusha chama wao wenyewe kutokana na chuki na kutokumaliza makundi ya uchaguzi.
Hayo aliyaeleza wakati wa kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na wasomi wa vyuo vikuu mkoani Mbeya, katika ukumbi wa Mtenda ambako yeye alikuwa mgeni rasmi.
' Tumekuwa mabubu, hatusemi mambo ambayo serikali inafanya, unafiki umezidi ndani ya chama na wengine wanachukia wakielezwa ukweli wakati chama chetu kinajipambanua kuwa ni muhimu kukosoana. Alisema Dr. Mary Mwanjelwa.
Picha na Kalulunga blog.
No comments:
Post a Comment