Social Icons

Thursday, 27 March 2014

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM KITAIFA MKOANI MBEYA YAENDELEA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Momba Ndugu Mwandusu

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa CCM Taifa na Mkoa wa Mbeya

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye akitoka uwanja wa ndege wa Songwe


Katibu Siasa na Uenezi Mkoa wa Mbeya Ndugu Bashiru Madodi akiwa katika harakati za maaandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM Jijini Mbeya.

Viongozi wa CCM wakiwa ofisi kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, kutoka kushoto ni Ndugu, Bashiru Madodi, Katibu Siasa na Uenezi Mkoa wa Mbeya, ndugu, Dogo Idd Mabruki, Makamu Mwenyekiti Wazazi Taifa, Dkt Mary Mwanjelwa Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Taifa.

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye akicheza draft na mmoja wa vijana katika Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye akipata chakula cha mchana kwa mama ntilie katika soko la Mwanjelwa jijini Mbeya

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye akishiriki katika ukarabati wa pich ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, uwanja huu unamilikiwa na CCM


Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Nape Nnauye akitoa maelekezo kwa katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema, wakati wa maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM

Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (CHADEMA)

                                                Habari na Basahama Blog












No comments:

 
 
Blogger Templates