Social Icons

Sunday, 20 April 2014

Kinana: Katiba mpya itapatikana

KATIBA MPYA LAZIMA IPATIKANE – KINANA
Licha ya madudu yanayofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana amewata Watanzania kuwa watulivu akisema ni lazima Katiba mpya itapatikana huku akisisitiza watambue kuwa Katiba hiyo si mwarobaini wa matatizo yaliyopo sasa hapa nchini. 

Kiongozi huyo akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku 20 katika mikoa minne, Dar es salaam ,Rukwa, Kigoma na Katavi ya kukagua utekelezaji wa ilani na kuimarisha chama hicho. Katika mkutano alikuwa akizungumzia matukio yanayoendelea kutokea Bunge la Katiba ambapo aliwatoa hofu Watanzania kuwa hayazuii kupatikana kwa Katiba hiyo kama iliyopangwa.Akitolea mfano nchi

ambazo zina Katiba bora duniani kama vile Afrika Kusini na Namibia ambazo hadi leo bado maisha ya wananchi wake yako vilevile kwa kuwa utekelezaji wa mwongozo huo unakwenda hatua kwa hatua. Alisema kinachoendelea kwa sasa bungeni ni wazi baadhi ya watu kutoka vyama vya upinzani akili zao zimejikita katika uroho wa madaraka na ndio maana wanang’ang’ania mfumo wa Serikali tatu wakiwa na imani kuwa huenda wakapata madaraka. 

Alibainisha kuwa chama hicho kimekuwa kikalaumiwa kuwa kinatawala maamuzi ya Bunge kutokana na wingi wa wabunge wake, jambo ambalo alikiri na kusisitiza kuwa wabunge hao hawakujipeleka wenyewe kwenye Bunge bali walichaguliwa na wananchi na maamuzi wanayotoa yanatokana na wananchi. Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema yanayoendelea bungeni kwa sasa yasiwasumbue akili wananchi kwa kuwa chama hicho kitahakikisha Katiba mpya yenye mtazamo na matakwa ya wananchi inapatikana. 

Alisema kitendo cha utawla kuanzisha migogoro na kutoka nje ya Bunge ni kutafuta umaarufu kutokana na ukweli kuwa tayari walishalipwa posho ya siku sita hivyo kutoka kwao kuwaathiri kimaslahi. Alisema kitendo cha UKAWA kuanzisha migogoro na kutoka nje ya bUnge ni kutafuta umaarufu kutokana na ukweli kuwa tayari walishalipwa posho ya siku sita hivyo kutoka kwao hakuwaathiri kimaslahi.

                                                       Basahama blog

No comments:

 
 
Blogger Templates