Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara.
Ndugu Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara wake uweze kuendelea na safari.
Sehemu korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanahabari aliokuwa ameambatana nao kwenye msafara wake,baada ya magari kunasa kutokana tatizo la barabara
Wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakiwa hoi kabisa,wakisubiri kudra za Mwenyezi Mungu,msafara wa magari yao yanasuliwe na kuendelea na safari.Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu,Ndugu Kinana.
Hali ilikuwa tete mnoo,kipande cha kilometa mia kinapitika kwa zaidi ya masaa sita,kutoka kijiji kimoja kwenda kingine.
Ilikuwa ni shughuli nzito katika msafara wa Ndugu Kinana,barabara ni mbovu kupita maelezo
Kila mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (anayerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe,ili msafara uweze kupita
Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi ya barabara kwa miguu,huku madereva wakipiga hesabu zao namna ya kupita.
Mchuma ukipita sehemu korofi ya barabara kwa mbinde.
No comments:
Post a Comment