Social Icons

Friday, 2 May 2014

Operesheni ya kijeshi yaanza katika mji wa Slovyansk, Ukraine

Jeshi la Ukraine linaripotiwa kuanza operesheni ya kijeshi kuudhibiti mji wa Mashariki mwa Ukraine wa Slovyansk.Kuna taarifa kuwa helikopta moja imedunguliwa katika mji huo

Shirika la habari la Ujerumani Dpa limeripoti kuwa helikopta mbili za kijeshi zimedunguliwa na rubani mmoja ameuawa huku mwingine akitekwa nyara.Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine na kujiunga na Urusi wamesema wanajeshi hao wameanzisha kile walichokiita operesheni kubwa katika mji wa Slovyansk.Milio ya risasi na miripuko imesikika viungani mwa mji huo.Serikali ya Ukraine haijazungumzia operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza muda mfupi uliopita.Mengi zaidi kuhusu hali inavyojiri mashariki mwa Ukraine ni hivi punde.

Chanzo:- Dw.de


No comments:

 
 
Blogger Templates