Social Icons

Friday 2 May 2014

WANASIASA KENYA WANA MAMBO

Huyu ndie amemtukana Rais na kusema aache Bangi kilichofuata ni hiki

Screen Shot 2014-05-01 at 4.09.41 PM 
Sio jambo la kawaida mtu kujiamini na kumtukana Rais wa nchi na taarifa hiyo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari lakini kwa Samuel Onkwami imekua rahisi kwake ila imemgharimu maana sasa hivi yuko kwenye sehemu atakayoshughulikiwa.

Ni mwakilishi wa Wadi ya Kiogoro Kaunti ya kisii huko Kenya na sasa amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kudai kwamba Rais Uhuru Kenyatta anavuta Bangi ambapo ishu ilianzia pale alipokaririwa Kanisani akihutubia na kusema ‘walio karibu na Rais Uhuru Kenyatta sharti wamshauri aache kuvuta Bangi’’

Kiongozi wa mashtaka ameiambia mahakama ya kisii kwamba mwakilishi huyo wa wadi alitoa matamshi hayo katika kijiji cha karera na sheria inayo mshtaki mtuhumiwa inasema ni hatia kwa yeyote kutoa matamshi kama hayo kuhusu mtumishi wa umma  .

Samuel ambae ni baba ya watoto watano anataaluma ya Teknolojia ya maabara kutoka chuo kikuu cha Teknolojia Mombasa na amewahi kuhudumu katika ofisi za hazina ya ustawishaji eneo Bunge kabla ya kuingia kwenye siasa mwaka wa 2007 na baadae kuchaguliwa mwaka uliopita kuwa mwakilishi wa Wadi.

Screen Shot 2014-05-01 at 4.34.08 PM
Mawakili wa mshukiwa ambao ni Gideon Nyambati na Isaiah Mosota wameiomba mahakama hiyo kumuachia huru mshukiwa kwa dhamana na kuomba upande wa mashtaka kuwapa ushahidi na malalamishi dhidi ya mteja wao ili kujiandaa vyema kwa ajili ya kutoa utetezi wao.
Mshtakiwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000 pesa za Kenya na Kesi hiyo itatajwa Mana kusikilizwa June 3 2014. Screen Shot 2014-05-01 at 4.27.10 PM

No comments:

 
 
Blogger Templates