Diwani wa Kata ya Bagamoyo Mhe. Bashiru Madodi (aliyeshika karatasi) akiwaonyesha wajumbe ramani ya soko la kata ya Bagamoyo
Diwani wa Kata ya Bagamoyo Mhe Bashiru Madodi (mwenye miwani) akiwaongoza wajumbe wa kamati ya soko kuwaonyesha mipaka ya eneo la soko
Diwani wa kata ya Bagamoyo akiwafafanulia jambo wajumbe
Diwani akiendelea na ufafanuzi wa mambo ya muhimu katika kuanzisha soko
Wajumbe wakiangalia eneo ambalo vitajengwa vibanda vya biashara
Wajumbe wakiendelea kupata ufafanuzi kutoka kwa diwani wao
Mwenyekiti wa CCM kata ya Bagamoyo Ndugu Ahmad Issah (kulia) akiwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Bagamoyo Bi. Neema Sarro
Mijadala ikiendelea wakati wa kunyeshana maeneo ya soko
Wajumbe wakiendelea kupata maelezo
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bagamoyo Bi, Neema Sarro (kulia) akiwa na wajumbe wa kamati ya soko.
Kata ya Bagamoyo inatarajia kuanzisha soko la kata katika kipindi kifupi kijacho, uongozi wa kata ya Bagamoyo leo ulikutana na wajumbe wa kamati ya uanzishwaji wa soko iliyo chini ya mama Mwalwama, Pia uongozi wa kata umewaonyesha wajumbe wa kamati hiyo ramani ya soko pamoja na mipaka ya eneo la soko.
Soko hilo linatarajiwa kuwa na vibanda vya maduka 40, sehemu ya kuuzia mitumba, sehemu ya kuuzia matunda na mbogamboga pamoja na sehemu ya kupaki magari makubwa, soko hilo litaanzishwa katika mtaa wa Batini eneo ambalo kwa sasa linatumika kama kilabu cha pombe za kienyeji.
Picha na habari na Basahama blog.
No comments:
Post a Comment