Jengo la zamani la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Jengo jipya la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakiwa katika mojawapo ya vikao vya baraza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi, Veronica Kessy
Jengo la zamani la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2013 / 2014 imetekeleza miradi mbalimbali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo, katika kipindi hicho Halmashauri imetumia kiasi cha Shilingi 6,311,832,955.96. Kwa kazi za maendeleo kwa mchanganuo ufuatao.
Miradi ya maji Shilingi 2,772,740,198.47, miradi ya barabara Shilingi 1,186,309,230.41, Miradi ya kilimo Shilingi 961,327,227.00, Basket fund Shilingi 299,042,200.00, LGCDG Shilingi 201,689,000.00, Nyumba za waalimu Shilingi 300,000,000.00, Madaraja Shilingi 100,000,000.00, DFID DEV F.Shilingi 175,454,307.00, SEDEP FUND Shilingi 129,775,656.00, Urban Local Government Shilingi 24,830,012.00, Fedha za jimbo Shilingi 82,016,507.00 na NMSF Shilingi 78,648,617.18
Pia halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetumia kiasi cha shilingi 16,855,202,176.78 kwa matumizi mengine kwa mchanganuo ufuatao. Mishahara Shilingi 13,115,735,665.05, Matumizi mengineyo OC Shilingi 2,592,034,114.04, na Matumizi kutokana na vyanzo vya ndani Shilingi 1,147,432,397.69.
Jumla ya fedha ilizotumia Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa mwaka wa fedha 2013 / 2014 ni Shilingi 23,167,035,132.74, kwa ajili ya kazi za maendeleo ikiwa ni pungufu ya Shilingi 9,885,626,032.74 ya fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kazi za maendeleo katika bajeti ya mwaka 2013 / 2014 ambazo zilikuwa ni Shilingi 33,052,661,170.00.
Kutokana upungufu wa fedha ambazo zilitakiwa kutumika katika shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, kuna baadhi ya miradi ambayo ilikuwa itekelezwe katika bajeti ya mwaka 2013 - 2014 imeshindikana kutekelezwa.
Hii ni taarifa iliyotolewa na katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe lililokutana tarehe 10.Julai 2014, katika ukumbi wa John Mwankenja.
Imetayarishwa na Bashiru Madodi
Basahama blogspot
No comments:
Post a Comment