Social Icons

Monday 8 September 2014

HADITHI: Missed call ya shemeji -4


“Mh!” aliguna dada mtu huyo huku akimwangalia shemeji yake kwa macho ya huruma…
“Sasa ina maana unaishije shemeji?”
“Kivipi shemeji?”
JIACHIE KIVYAKO…

Aaaa! Masuala fulani…”
“Kama..?”

“Kamaa…aaa…da! Yaani inapotokea mmegombana kama wanandoa inakuaje usiku, anakuchia uhuru au anabana?”

“Mh! Shemeji we acha tu, mdogo wako ananibania sana. Si inapotokea tumegombana tu, hata kama hatujagombana. Kwa kawaida yeye mpaka ajisikie…
“Mbaya zaidi shemeji, hata inapotokea mimi naumwa halafu yeye anataka ananilazimisha, lakini kwa upande wake sivyo.” 

“Da! Jamani, Aisha ameipatia wapi hiyo tabia? Sisi hatujalelewa hivyo, ndiyo maana hata siku ya harusi kama unakumbuka shemeji, baba aliongea sana, alimwambia akaishi na mumewe kwa jinsi alivyolelewa…

“Tena shemeji kama utakumbuka vizuri, baba alisema kusalitiwa ndani ya nyumba kunatokana na mke mwenyewe, ndiyo kama hivi. Sasa kwa mfano ukitaka kumsaliti hapa atasema wewe si mwaminmifu? Si yeye mwenyewe ndiye atakuwa chanzo?”

“Ni kweli shemeji, labda uongee naye mdogo wako.”
“Akha! Niongee naye nini? Yeye si mtoto, anajua maisha, anajua kila kitu, mtoto ukimnyima chakula ndani akienda kula kwa majirani utamsema?”
“Huwezi kumsema shemeji!”

“Huwezi kabisa, maana wewe ndiye tatizo,” alishadadia dada wa Aisha.

Beka akaendelea kulalamika…
“Unajua shemeji ilifika mahali nikasema afadhali ningekuoa wewe, maana kama unakumbuka wewe ndiye ulikuwa wa kwanza kuonana na mimi nilipokuja kule kikazi, ndiyo nikasikia ulikwenda likizo na ulikuwa una mume.”

“Wewe kama mimi shemeji, hata wakati wa matatizo na mume wangu nilisema moyoni afadhali ningeolewa na wewe, unaonekana ni mtulivu, mvumilivu na mwingi wa busara kama siyo hekima.”
Mara mlio wa gari ulisikika kwa nje, Aisha alikuwa amerejea…
“Shemeji huyo mwenye mji amerudi, baadaye basi shemeji,” alisema dada wa Aisha kwa sauti ya kuiba asisikike huku akiwa amesimama…

“Sasa shemeji mazungumzo yetu bado lakini, nipe namba ya simu…”


Nitakupa kiaina,” alisema dada mtu huyo huku akitokomelea chumbani kwake kwa mwendo wa haraka kama vile alikuwa hataki akutwe akiwa laivu na shemeji yake.
“Za saa hizi?” Aisha alimsalimia mumewe…
“Salama tu, za huko?”

“Huko poa kiasi chake, lakini si sana.”
“Kwa nini?”

“Nimechoka sana, leo mambo yalikuwa mengi sana mume wangu.”
Wakati Aisha anatumia neno ‘mume wangu’, Beka akakumbuka jambo aliloongea na shemeji yake…
“Akha! Niongee naye nini? Yeye si mtoto, anajua maisha, anajua kila kitu, mtoto ukimnyima chakula ndani akienda kula kwa majirani utamsema?”


Huwezi kumsema shemeji.”
“Pole sana mke wangu,” alidakia Beka huku moyoni akisema…
“Ningekuwa mumeo kweli ungekuwa unaninyanyasa kitandani?”
“Nimeshapoa mume wangu! Dada yuko wapi?”
“Nadhani chumbani kwake.”
“Amelala?”

“Sijui, lakini alikuwepo.”
“Au anaumwa?”
“Nimekwambia sijui mke wangu.”
Aisha alipita hadi chumbani kwa dada yake akamkuta amelala kitandani lakini si usingizi…
“Dada shikamoo.”

“Marahaba, pole na majukumu mdogo wangu.”
“Nimepoa, ulikula mchana?”
“Aaah! Nilikula sana, tena nilishiba haswa sidhani kama usiku nitakula.”
“Kwa nini usile? Yaani kula mchana ni sawa na kula usiku? Mbona kila mlo unajitegemea.”
“Tatizo shibe mdogo wangu.”
“Hamna bwana dada, usiwe hivyo, lazima ule hata siku shemeji akikuona ajue kweli ulikuwa ukitunzwa na mdogo wako.”

Wakacheka, Aisha akatoka huku dada yake akimwangalia kwa nyuma na kusema moyoni…
“We cheza na mume tu, siku moja utajikuta unalia kilio cha mbwa, mdomo juu, masikio walu, mjini hapa! Ohoo!”

Aisha alikwenda kubadili nguo, alipotoka alikaa sebuleni na mumewe Beka wakizungumza na mambo mawili matatu kisha akaenda jikoni kuanza maandalizi ya chakula cha jioni.

***
Kule chumbani, baada ya kuondoka Aisha, dada mtu aliwaza kitu…
“Hivi, mimi na shemeji tutamaliza salama kweli? Mbona kama viashiria fulani si vizuri? Ina maana na yeye…mh! haya, tupo hapa,” alisema moyoni akiwa amekaa kitandani na kujiinamia kwa mawazo…
“Lakini kwa mfano sasa, imetokea mambo yamekwenda mwisho wake yamekuwa mambo, itakuaje? Nikubali? Noo! Siwezi kumkubalia shemeji yangu, yule ni mume wa mdogo wangu wa damu moja…

“Lakini sasa anamtesa mumewe, anamnyima haki yake ya ndoa, anasema mpaka apende yeye, ikitokea akapenda mume yeye hataki majanga.”

***
Jikoni na sebuleni ni mbali kidogo, dada mtu alitoka chumbani kwake akaenda kuungana na mdogo wake jikoni kwa ajili ya maandalizi ya chakula.

Ndipo alipokumbuka kwamba, aliahidi kutoa namba yake ya simu kwa shemejiye, hivyo akaenda chumbani kwake na kuchukua kalamu na karatasi akaiandika namba hiyo na kukikunja kile kikaratasi na kutembea nacho hadi sebuleni, akamtupia shemeji yake na kuondoka zake kurudi jikoni.

“Majangaa…majangaa…mbona majangaaa…mbona majangaa…,” aliimba dada mtu huyo, mdogo wake akapokea…

“Ndoa nifunge mimi, fungate niende mimi, mume umchukue wewee…kuolewa niolewe mimi, mahari nitolewe mimi, mume uite wewe,” alidakia Aisha huku akicheka…
“Majangaa…majangaa…mbona majangaa,” aliendelea kuimba dada mtu kwenye eneo la kibwagizo cha wimbo huo kisha wote wakacheka sana, ghafla dada mtu akasema...

Itaendelea,

Chanzo: globalpublishers

No comments:

 
 
Blogger Templates