Social Icons

Monday 13 October 2014

Taifa Stars yaisasambua Benin 4 - 1 uwanja wa Taifa

Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars,Juma Luizio akiipachikia bao nne timu yake katika mtangange wa kikataifa wa kirafiki dhidi ya Benin,uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda 4-1 dhidi ya Benin.
 Wachezaji wa Taifa Stars,wakishangilia ushindi wao huku wakiwaacha wapinzani wao wa Benin wakiwa hoi tena wakiwa hawaamini wanachokiona uwanjani hapo.
 Washabiki wa Taifa stars wakiisapoti vilivyo timu yao.
 Ubao wa ulionyesha hivi kabla jamaa hawajapata la kufutia machozi.
 Shangwe tupu ilikuwa uwanjani hapa.
 Dogo muokota mipira akiisikilizia baridi iliyoambatana na kimvua cha kiaina.
 Uzalendo ndio mpango mzima,pamoja na kwamba mvua ilikuwa ikinyesha lakini hakuna alietaka kuondoka uwanjani hapo hasa kutokana na burudani safi iliyoonyeshwa na Taifa Stars leo.Picha na Othman Michuzi.,MMG.

No comments:

 
 
Blogger Templates