Kadi bandia za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya zimekamatwa siku chache baada ya mchakato wa kura za maoni kumalizika.
Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Mbeya, Bashir Madodi amesema kuwa wamebaini uwepo wa kadi nyingi bandia katika mkoa huo baada ya kuwepo ongezeko la kadi mpya ambazo hazikutoka katika makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa kadi hizo zimekuwa zikitumika katika kufanya hujuma katika michakato mbalimbali ya uchaguzi wa kura za maoni.
Akizungumzia kadi hizo amesema Bashir amesema Kwa kawaida kadi zinatoka makao makuu, zikifika hapa mkoani zinasajiliwa. Namba zikishasajiliwa ndipo zinapelekwa wilayani. Sasa kuna kadi nyingi ambazo zinaonekana ambazo hazikusajiliwa katika mkoa wetu. Kwa hiyo zile kadi sio halali kwa mkoa wetu.
Katika hatua nyingine Chama hicho kimedai kuwa kadi hizo bandia ndizo ambazo hutumiwa na vyama vya upinzani kutengeneza propaganda ya kisiasa na kuonesha kuwa wana CCM wamerudisha kadi nyingi.
No comments:
Post a Comment