MAPOROMOKO YA MAJI KAPIKI/ KAPIKI WATERFALLS
Maporomoko ya maji Kapiki yanapatikana Mkoani Mbeya katika Wilaya ya Rungwe kijiji cha Mboyo, Ni moja kati ya vivutio vikubwa na vizuri sana lakini havijatangazwa ili kufahamika kwa wadau, ungana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES katika kampeni yetu endelevu ya kutangaza na kuelimisha umma juu ya vivutio mbali mbali vya kitalii vipatikanavyo mkoani Mbeya.

Maporomoko haya yanapatikana katika mto uliobeba maajabu kadhaa ikiwemo Daraja la Mungu Kiwira, Kijungu Jiko, N.k kuanzia katika chanzo chake mpaka unapo mwaga maji yake ziwa Nyasa si mwingine ni Mto Kiwira.
Kwa kutizama kwa macho twaweza kusema yakawa ndio maporomoko marefu kwa Wilaya ya Rungwe (japo haijathibitishwa kitaalam) kutokana kwamba ukiyatizama yanayazidi yale ya Malasusa, na Kaporogwe pia. Kwa mujibu wa mwenyeji wetu alisema inasemekana nyuma ya poromoko hili kuna shimo (pango) ambalo linakwenda umbali fulani japokuwa yeye hajawahi kuingia.
Kuna sehemu nzuri ya kuangalizia hasa kipindi ambacho si cha mvua kwani kipindi cha mvua maji hupita sehemu hiyo, lakini pia hali ya hewa ni safi na mwanana
Shukrani za dhati kwa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kupitia kitengo cha utalii, kwa ushirikiano mkubwa mliotupa na hata kufanikisha hili.
Tunawaomba wana mbeya muzidi kutangaza vivutio vya kitalii vilivyoko kwenye mkoa wa Mbeya, katika blog mbalimbali.
For details and booking, contact the tour coordinator through;
Mobile: +255 (0) 783545464/766422703
Email: uyolecte@gmail.com, Blog: uyolecte.blogspot.com
Facebook: www.facebook.com/uyoculturaltourismenterprises
Instagram: @uyoleculturaltourismenterprise
Mobile: +255 (0) 783545464/766422703
Email: uyolecte@gmail.com, Blog: uyolecte.blogspot.com
Facebook: www.facebook.com/uyoculturaltourismenterprises
Instagram: @uyoleculturaltourismenterprise

No comments:
Post a Comment