WANAFUNZI SABA WAJERUHIWA KUFUATIA UPEPO MKALI KUEZUA PAA LA SHULE
Na Editha Karlo, wa blog ya jamii,Missenyi
SHULE ya msingi Byamutemba iliyopo katika kata ya Nsunga Wilayani Misenyi imefungwa kwa muda wa wiki tatu,kufuatia shule hiyo mapaa yake kuezuliwa na upepo mkali.
Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana wakati wanafunzi wakiendelea na masomo darasani na kusababisha baadhi ya wanafunzi kujeruhiwa.Upepo huo umeezua mapaa ya shule hiyo nyumba moja ya mwalimu pamoja na nyumba tatu za wakazi wa kijiji cha Byamutemba.
Mganga msaidizi wa Wilaya ya Missenyi Godon amekiri kupokea wanafunzi hao waliojeruhiwa 14 na wanafunzi 7 wakirudishwa nyumbani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Zahanati ya Igayaza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila alisema kuwa wameifunga shule hiyo kwa miezi mitatu wakati wanafanya utaratibu wa kuijenga shule hiyo kwa haraka.
Alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 903.
Shule ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi imeezuliwa na upepo mkali na kupelekea Wanafunzi saba kujeruhiwa,kufuatia tukio hilo, shule hiyo kwa sasa imefungwa kwa muda.





No comments:
Post a Comment