Trump Trump Trump kila kona ya dunia linatajwa jina la Donald
Trump wengi wakishangaa amepataje urais wakati hata viongozi wengi wa chama chake walikuwa hawamuungi mkono?
Yapo mawazo ya watu wengi sana wanaoamini kuwa siasa nzuri za marekani ni za chama cha Democratic na sio Republican ukweli ni kwamba wamarekani ni wamoja na ni kitu kimoja muda wote.
Wameviweka vyama hivi makusudi ili kuihadaa dunia na kila chama kimepangiwa majukumu yake ili kufanikisha mchezo wao wa kuitawala dunia na kwa kweli wamefanikiwa sana katika hili.
Ngoja nikusimulie kidogo siasa za marekani kwa uelewa wangu mdogo tu, mimi nimekuwa nikifuatilia siasa za marekani tangu mwaka 1974 pale ambapo aliekuwa rais wa marekani Gerald Ford alipomuandikia barua aliekuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, na kumtaka rais wetu achague kama yupo tayari kuwa awekwe kwenye orodha ya maadui wa marekani.
Ambao ni USSR, China, Cuba, Mongoria, Korea kasikazini, Ribia na Ujerumani mashariki, jambo lilinishangaza sana kwamba marekani ina mamlaka gani kwa nchi yetu kiasi cha kutoa amri hii?
Tangu vita vya pili vya dunia vilipomalizika mwaka 1945, Marekani ilikuwa na hofu kuwa asiibuke mtu au nchi yeyote inayoweza kuitishia dunia tena kama ilivyokuwa kwa Ujerman na marafiki zake, ikachukuwa hatua za kuunda kambi yake ya kujihami ya magharibi na kuanzisha shirika la kujihami NATO na shirika ujasusi la CIA, kwa upande wa pili kwa maana ya kambi iliyokuwa linaongozwa na USSR Ulaya mashariki na kuunda chombo cha kujihami kikiitwa Warsal park na shirika la ujasusi la KGB kazi ya shirika hili ni kupambana na magharibi na ubepali popote pale.
Mashirika haya ya CIA na KGB yalikuwa ni kushindana na atakaeshinda ndo aiongoze dunia kwa mjibu wa sera zao, katika kipindi chote tangu mwaka 1945 kila mmoja alikuwa na hofu na mwenzake na ndo maana kulikuwa na kitu kinaitwa vita baridi kati ya magharibi na mashariki vita hivi vilidumu mpaka mwaka 1980, alipochaguliwa Rais Ronald Regan ambae aliibadirisha marekani kwa kuongeza nguvu kubwa ya kuishinda USSR, na hatimae kubomoa ukuta wa Berlin mwaka 1989 ndipo nguvu za USSR zikaishia na kuvunjika vipande vipande mataifa 15 yaliyokuwa yaunda USSR kila moja lilijiundia mamlaka yake yenyewe na sehemu kubwa ya mataifa yalijiunga na NATO.
Ikumbukwe kuwa wamarekani wao wanajiona ni Taifa kubwa na wanajivunia fahari yao kuliko taifa lolote na wanajivunia Taifa lao.
lakini hawataki kabisa vita ipiganiwe katika nchi yao, ni kwa nini USSR ilishindwa katika vita baridi? CIA ilikuwa imetandaa sana duniani kote kutokana na uwezo wake wa kiuchumi kwa maana wao walikuwa na uweza wa kupenya popote hata ndani ya maadui zake kupitia nchi au mtu wa tatu lakini pia uhodari wa kuwa ndumila kuwili.
Hakika wamarekani ni mabingwa wa unafiki wanauma na kupuliza, Ikumbukwe kuwa wamarekani hawana rafiki wa kudumu na wala hawana adui wa kudumu.
Marekani wamejitahidi kuwa na marafiki wengi, na baadae wakaamua kuwaacha njiani baada ya kuona malengo yao yametimia au kwa wakati huo yamechuja kwengi tunakumbuka jinsi Jonas Savimbi wa chama cha UNITA alivyokuwa rafiki yake mkubwa, Joseph Mabutu wa DRC, Idd Amin dada wa Uganda, Jafar Nimer wa Sudan, Sadam Husein wa Iraq na Osama bin Laden na wengine wengi ambao sijawataja inaonyesha ni jinsi gani Marekani walivyo na unafiki hawa ni baadhi tu lakini wapo wengi sana.
Hapo juu nimekueleza jinsi Sadam Hussein alivyochukuliwa kutoka sajent kikosi cha ulinzi wa mfalme na kuwa mkuu wa nchi na nchi yake kujengewa uwezo mkubwa wa kivita nia ilikuwa ni kupambana na Iran ambayo alikuwa rafiki mkubwa wa marekani baada ya Israel katika mashariki ya kati kimsingi hakuna mahali penye mgogoro ambapo marekani haijashiri tena huwa wanashiriki pandezote mbili moja kwa moja au kupitia nchi ya tatu.
Sasa ni kwa nini Trump na asiwe Clinton? Sasa ngoja nikusimulie kidogo katika hili, wamarekani wanacheza na dunia wanamuweka rais ili kulinda maslahi yao lakini pia Taifa la Israel lina nafasi yake katika siasa za marekani kama mnafuatilia vizuri utagundua kuwa vita vya Iraq Israel iliisukuma marekani kuibomoa kutokana na kitisho kikubwa cha Sadam Husein kuwa na nguvu kubwa za kijeshi kiasi kwamba ilifikia kuwa nchi ya nne duniani kuwa na nguvu za kijeshi baada ya marekani, Urusi, Uchina kwa kuwa siku moja waziri mkuu wa Israel alitamka kuwa wao wako hatarilini kuangamizwa na Iraq kwa kuwa marekani wameiwezesha sana kivita na akasema Israel ikiteketea marekani watabeba lawama.
Na kwa bahati mbaya Sadam aliwahisema kuwa ataiteketeza Israel, pia ikumbukwe kuwa Rais wa marekani amepewa nguvu za ziada kama kuna jambo ambalo linaharisha usalama wa marekani ikiwa ni pamoja na Israel, kwa msingi huo anatakiwa rais mwenye msimamo mkali na mwenye kusimimia vilivyo maslahi ya wamarekani ndo maana akachaguliwa George Bushi (mtoto), ambae alikuwa mkurugenzi wa CIA hata kama alipatikana kwa figisu figisu jambo ambalo ingekuwa kwetu ilikuwa shida lakini wao wanaangalia maslahi ya taifa lao.
Baraka Obama alipatikana baada ya vita vya Iraq wengi mnafahamu kuwa vita vile viliichafua sana marekani kiasi kwamba marafiki zake wengi walianza kumshuku kuwa sio rafiki mwema, ilibidi apatikane rais ambae hatatiliwa shaka wote mnakumbuka kuwa Afrika ilizizima kuwa wamepata mkombozi wao hata nchi za kiarabu zilifurahia ujio wa Obama lakini huo ulikuwa ni unafiki wa marekani tu, na kwa kweli alikuja na lugha tamu sana tukalaghaika sana ila kwangu mimi naona hakuna jipya alilolifanya kwa Afrika.
Katika kipindi hiki cha utawala wa Obama wengi mnafahamu kuwa Rusia imekuja juu katika maeneo mbali mbali angalia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Siria, Chechenia na maeneo mengine mengi kiasi kwamba imeanza kuzuka hofu kwa wamarekani kuwa USSR inaibuka tena na ni lazima apatikane mtu mwenye nguvu anaejua vizuri maslahi ya Marekani na mwenye uwezo wa kubadilika badilika kama alivyokuwa Reonald Regan kwa maslahi ya Taifa lao, CIA na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vikapanga mkakati wa namna ya kumpitisha Trump alieonekana kuwa kwa sasa ndie chaguo lao na kuingia ndani ya chama cha Repulican kwa sababu mwanzo alikuwa mwanachama wa Democratic, kumbuka waliogombea walikuwa zaidi ya 15 na wengine walikuwa wazuri sana kuliko Trump pia walikuwa wanaongoza kwenye kura za maoni, ndani ya chama chao lakini ghafla walianza kujitoa mmoja baada ya mwingine lakini kubwa zaidi ni viongozi na watu mashuhuri kutangaza kuwa hawamuungi mkono Trump hiyo ilikuwa ni laghai ya kuwafanya Democratic wajiaminishe kuwa wao ni washindi.
Vyombo hivi vilipenya ndani ya chama cha Demoratc na kufanikiwa kuwalaghai wasifanye kampeni ipasavyo ili ashinde kwa kura sio kwa kwa ujanja ujanja kama ilivyokuwa kwa Bushi (mtoto), Trump alionekana yupo peke yake alitumia maneno makali yanaoyoonyesha uzalendo halisi jambo ambalo wamarekani wanalipenda mno hakuna mahali ambapo hakuenda kufanya kampeni kinyume na Clinton ambae maeneo mengi alituma wawakilishi na muda wote Trump aliogozwa na vyombo hivi ili kumhakikishia ushindi.
Sote tumeoshuhudia ushindi usio na shaka, hakika marekani ina wenyewe tafauti na sisi wa nje tunavyofikiri wala haikuwa bahati mbaya kuanguka Crinton ilikuwa imepangwa.
Kwa msingi huo kila Taifa lina misingi yake ya namna ya kuchaguana na kuongozwa kwa kuzingatia mazingira na maslahi yake wenyewe.
Nimesema kwa uchache tu, ili kutoa nafasi ya wengine kufuatilia kwa undani kujazia hapa.
Imeandikwa na:
Edson Mwaibanje, mwaibanjeedson@yahoo.com

No comments:
Post a Comment