Waziri wa maswa la ya kigeni nchini Qatar amekataa orodha ya mahitaji 13 yaliotolewa na mataifa manne ya kiarabu ili taifa hilo liondolewe vikwazo akisema sio busara na wala haiwezekani
Saudia ,Misri, UAE na Bahrain yameiwekea Qatar vikwazo vikali na kutoa orodha ya masharti 13 ambayo inafaa kuafikia kabla ya vikwazo kuondolewa.
Shirika la habari la AL Jazeera linalofadhiliwa na Qatar limeyashutumu mataifa ya kiarabu yanayotaka lifungwe.
''Mahitaji hayo ni jaribio la kuingilia uhuru wa kujieleza''lilisema.
- Madhara yatakayoletwa na kuitenga Qatar
- Qatar yaapa kutosalimu amri Uarabuni
- Mataifa ya Kiarabu yajitenga na Qatar
- Qatar yanunua ndege za kivita kutoka Marekani
Pia mataifa hayo yanataka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran mbali na kufunga kambi ya jeshi la Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.
Hatua hiyo inajiri baada ya wiki mbili za vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Qatar ikiwa ni mzozo mbaya zaidi wa kisiasa miongoni mwa mataifa ya Ghuba kwa miongo kadhaa.
Qatar ambayo inataka kujiimarisha katika siku za hivi karibuni imekana madai kwamba inayafadhili makundi ya kigaidi mbali na kusababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
Katika taarifa ,Al Jazeera imesema ,'' tunasisitiza haki yetu ya kuendelea kutoa habari kwa hali ya kitaalam bila ya shinikizo zozote kutoka kwa serikali yoyote ama mamlaka.
- Mataifa 4 ya kiarabu yaipa Qatar masharti 13 kuafikia
- Qatar kutumia pesa nyingi kuandaa Kombe la Dunia
- Kundi la Hamas lapata kiongozi mpya
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-thani alisema awali kwamba nchi yake haitajadiliana hadi vikwazo hivyo viondolewe.
Pia amekana kwamba taifa lake linafadhili shirika lolote la kigaidi .
Anwar Gargash waziri wa maswala ya kigeni katika milki za kiarabu UAE alichapisha ujumbe wa Twitter akisema: Ni muhimu kwa Qatar kaufikia masharti hayo mbali na wasiwasi wa majirani zake kwa umuhimu mkubwa.
La sivyo tuipatie nchi hiyo talaka.
Chanzo. BBC
No comments:
Post a Comment