Urusi mwenyeji wa kombe la mabara imeanza vizuri jana baada ya kuishinda New Zealand kwa mabao 2-0.
Wachezaji wa Urusi ambao wengine hata hawafahamiki nje ya nchi yao walilazimisha bao la kwanza lililofungwa na mchezaji wa New Zealand Michael Boxal katika dakika ya 31, na mshambuliaji Fyodor Smolov aliongeza bao la pili katika dakika ya 69.
Timu zote zilisimama uwanjani wakisikiliza hotuba iliyotolewa na rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa shirikisho na kandanda duniani Gianini Infantino , kabla ya kuruhusiwa kukamilisha maandalizi ya pambano hilo.
Siku chache kabla , Putin aliwataka wachezaji wa timu hiyo kupata matokeo mazuri ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa Urusi.

Rais wa FIFA Gianini Infantino na rais wa Urusi Vladimir Putin katika michuano ya kombe la mabara mjini St. Petersberg, Urusi
Leo ni kati ya Ureno mabingwa wa bara la Ulaya dhidi ya Mexico.
Mwandishi : Sekione Kitojo / ape
Chanzo. Dw.de


No comments:
Post a Comment