Social Icons

Sunday, 28 January 2018

Kenyatta ateua mawaziri wapya Kenya, na balozi mpya Tanzania

Uhuru KenyattaHaki miliki ya pichaUHURU KENYATTA, FACEBOOK

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana.

Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi.

Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania.

Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.

Alishindwa kwenye uchaguzi huo.

Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi.

Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva.

Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu.

Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi

  • Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa
  • Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa Mataifa mjini Geneva
  • Dan Kazungu (Madini) - Tanzania
  • Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya
  • Willy Bett (Kilimo) - India
  • Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris
  • Hassan Wario (Michezo) - Austria

Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni:

  1. Adan Mohammed - Viwanda
  2. Amina Mohammed - Elimu
  3. Charles Keter - Kawi
  4. Eugene Wamalwa - Ugatuzi
  5. Farida Karoney - Ardhi
  6. Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama
  7. Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu)
  8. James Macharia - Uchukuzi
  9. John Munyes - Madini na Mafuta
  10. Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  11. Keriako Tobiko - Mazingira
  12. Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma
  13. Monica Juma -Mambo ya Nje
  14. Mwangi Kiunjuri - Kilimo
  15. Najib Balala - Utalii
  16. Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki
  17. Racheal Omamo - Ulinzi
  18. Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa)
  19. Rashid Achesa - Michezo
  20. Sicily Kariuki - Afya
  21. Simon Chergui - Maji
  22. Ukur Yattany - Leba

Chanzo. BBC

No comments:

 
 
Blogger Templates