Warusi wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa rais Jumapili (18.03.2018) unaotarajiwa kumpa Putin ushindi mkubwa ambao unaweza tu kuchafuliwa iwapo watu wengi hawatajitokeza kupiga kura kwa sababu matokeo yanatabirika.
Katika eneo la mashariki mwa Urusi, katika mji wa pwani ya bahari ya Pacific wa Petropavlovsk-Kamchatsky, vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema saa tano usiku saa za Urusi, na upigaji kura utaendelea katika nchi hiyo kubwa hadi vituo vitakapofungwa katika eneo la magharibi kabisa mwa nchi hiyo katika jimbo la Kaliningrad , masaa 22 baadaye.
Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unampa Putin , rais wa sasa , uungwaji mkono wa kiasi ya asilimia 70, ama karibu mara 10 zaidi ya uungwaji mkono wa mgombea anayemkaribia. Muhula mwingine utamchukua karibu robo karne akiwa madarakani, muda mrefu zaidi miongoni mwa viongozi wa serikali ya Kremlin wapi tu kwa dikteta wa enzi wa Kisovieti Josef Stalin.
Wengi wa wapiga kura wanamsifu Putin, mwenye umri wa miaka 65 jasusi wa zamani wa shirika la kijasusi la Urusi , KGB, kwa kutetea masilahi ya Urusi katika dunia hii yenye uhasama, hata kama gharama ni mapambano dhidi ya mataifa ya magharibi.
Mzozo na Uingereza kuhusiana na madai kwamba Kremlin ilitumia sumu inayoathiri mishipa ya fahamu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi katika mji mtulivu wa Uingereza , madai ambayo Urusi inakana , haujachafua uungwaji wake mkono.
Wengi wa wapiga kura hawaoni mtu mbadala kwa Putin, ana udhibiti kamili wa medani ya kisiasa pamoja na televisheni ya taifa, ambako watu wengi wanapata taarifa zao, na kutoa muda mkubwa kwa matangazo yanayomhusu Putin na muda mchache kwa wagombea wengine.
"Putin ndio rais wetu. Tunajivunia," amesema Marianna Shanina, mkaazi wa jimbo la Crimea. Urusi ililinyakua jimbo la Crimea kutoka Ukraine miaka minne iliyopita, na kumpa sifa Putin kutoka kwa Warusi wengi na shutuma kutoka mataifa ya magharibi.
Warusi hawana mbadala kwa Putin
"Tunamtakia ushindi katika uchaguzi. Familia yetu yote itampigia kura Putin. Putin ! Afya njema kwako, rais wetu mpenzi !," Shanina alisema katika mkutano wa kampeni wa Putin.
Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura uliofanywa Machi 9 na kampuni inayomilikiwa na serikali ya VTsIOM ilimpa Putin ambaye alichaguliwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka 2000, uungaji mkono wa asilimia 69. Mgombea aliyeko karibu nae Pavel Grudinin , mgombea wa chama cha Kikomunist , atapata asilimia 7.
Mjumbe wa tume ya uchaguzi nchini Urusi akiweka karatasi inayoonesha picha za wagombea katika uchaguzi nchini Urusi
Mwanasiasa wa kwanza katika miaka kadhaa kutoa changamoto kwa udhibiti wa serikali madarakani, Alexei Navalny, amezuiwa kushiriki katika uchaguzi huo kwasababu ya kuhumumiwa kwa madai ya rushwa, madai ambayo anasema alibambikiwa na serikali.
Anatoa wito wa kuususia uchaguzi huo, akisema ni kichekesho cha kitokuwa na demokasia, na kuwaweka waungaji wake mkono kukusanya ushahidi wa mtu yeyote atakayefanya udanganyifu katika uchaguzi kuweka idadi ya juu ya watu watakaoshiriki katika uchaguzi huo na uungwaji mkono wa Putin.
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny ambaye amezuiwa kugombea katika uchaguzi huo akikamatwa na poilisi, Januari 28, 2018
Serikali ya Urusi pembeni inakiri kuwa na wasi wasi kwamba baadhi ya Warusi milioni 110 wenye haki ya kupiga kura hawatajisumbua kupiga kura kwasababu wanaamini Putin atashinda tu. Uchache wa watu watakaojitokeza kupiga kura utaathiri mamlaka yake katika muhula ujao, ambao , chini ya katiba, utakuwa wa mwisho.
Katika hotuba kwa taifa iliyotangazwa moja kwa moja na televisheni ya taifa siku ya Ijumaa, Putin alisema wapigakura wana mustakabali wa nchi hiyo katika mikono yao.
Chanzo Dw.de
No comments:
Post a Comment