MWENYEKITI WA CCM TAIFA AZINDUA BARAZA LA USHAURI LA WAZEE WA CCM MKOANI DODOMA LEO
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM Mkoani Dodoma,tayari kwa ufunguzi wa baraza la ushauri la Wazee wa Chama,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma ndugu Adam Kimbisa.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, na Makamu Mwenyekiti Bara Mstaafu John Samuel Malecela, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Ndugu Benjamin William Mkapa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ndugu Aman Karume wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Wasanii wa Kundi la Kyela Beats wakitumbuiza wakati wa sherehe za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, leo Agosti 24,2013.
Katibu wa CCM Taifa ,Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za utangulizi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la CCM.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu pamoja na wanachama wa CCM wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wa Chama wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
No comments:
Post a Comment