NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA RASMI "DUTY FREE SHOP" YA KISASA GEREZA KARANGA, MOSHI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(wa pili kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima kabla ya kumkaribisha kuzindua rasmi Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( kulia) akiangalia jiwe la msingi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akiangalia baadhi ya bidhaa zitakazokuwa zikiuzwa katika Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013 mara baada ya uzinduzi rasmi huku akiwa ameongozana na Meneja wa Duka hilo pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mkoa wa Kilimanjaro na Wakurugenzi wa Transit Military Shop mara baada ya uzinduzi rasmi.
No comments:
Post a Comment