(DIWANI ATUMANI – ACP) KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA KYELA – MAUAJI. MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:30 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA 70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA KUPIGWA JIWE UBAVUNI NAANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA SAA 05:30 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUUASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA. Signed by: (DIWANI ATUMANI – ACP) KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment