[ DIWANI ATHUMANI - ACP ] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA MOMBA – WATU SABA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI NA KUJERUHI.
MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MCHANGANIKIJIJI CHA SENGA KATA YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKA KATIKA KIJIJI CHA ILAMBOKATA YA KAPETA WILAYA YA SUMBAWANGA VIJIJINI MKOA WA RUKWA WALIVAMIA MAKAMBI YA WAVUVI YALIYOPO KATIKA KIJIJI HICHO NA KUWAPIGA KWA KUTUMIA FIMBO KISHA KUCHOMA MOTO MABANDA KADHAA YA WAVUVI YALIYOJENGWA KWA KUTUMIA NYASI.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI KUGOMBEA ENEO LA VIJIJI TAJWA. UFUATILIAJI WA MGOGORO HUU UNAENDELEA. JUMLA YA WATU SITA WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MSABAHA S/O JUMA, MIAKA 40, MZARAMO,MKULIMA/MVUVI 2. MAXIMO S/O MWAKANYEMBA, MIAKA 24,KYUSA,MKULIMA/MVUVI 3. MICHAEL S/O SANGA, MIAKA 30,MKINGA,MKULIMA/MVUVI 4. CHONDE S/O KALISTO, MIAKA 56, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI 5. ZAWADI S/O JOHN SICHULA, MIAKA 39, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI NA 6. GIBSON S/O EDWARD KACHINGWE, MIAKA 26, MSAGALA, MKULIMA/MVUVI WAHANGA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA NA WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
KUFUATIA TUKIO HILO JUMLA YA WATUHUMIWA SABA WAMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI AMBAO NI 1. SAMWEL S/O DAUD, MIAKA 42, MNYIHA, MKULIMA 2. GERVAS S/O LUKAS, MIAKA 52, MSUKUMA, MKULIMA 3.NYERERE S/O MWITA, MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA 4.RICHARD S/O WILSON, MIAKA 43, MFIPA, MKULIMA 5. GEBRUS S/O RAMADHAN, MIAKA 28, MNYASA, MKULIMA 6. LULINDE S/O DASE, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA NA7. FUNGUZA S/O MASANJA, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA KAMSAMBA. KWA SASA HALI NI SALAMA KATIKA ENEO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WENGINE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 23.08.2013 MAJIRA YA SAA 10:35HRS HUKO KYELA- KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KAMWELA S/O MWASAMWENE,MIAKA 37,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA NANE [08] AKIWA AMEBEBA KWENYE BAISKELI YAKE. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 23.08.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA DEMARK S/O RAFOE,MIAKA 28,RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJII. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KUHUSU WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment