Timu ya Mbeya City
Timu ya Kagera Sugar
Mashabiki wa Mbeya City
Ligi ya Vodacom leo imefungua pazia nchini, katika Jiji la MbeyaTimu za Mbeya City na Kagera Sugar leo zimechuana vikali katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Katika mchezo huu timu zilishambuliana kwa za zamu na mpaka zinakwenda mapumziko, timu ya Mbeya City ilikuwa imepoteza nafasi nyingi za kujipatia mabao ya kuongoza, hata hivyo mpaka timu zinakwenda mapumzikoni hakuna timu iliyokuwa imepata bao.
Kipindi cha pili timu ziliingia uwanjani kwa kasi na kushambuliana kwa zamu, hata hivyo timu ya Mbeya City itabidi ijilaumu sana kwa kukosa ushindi katika mchezo wa leo, kwani walipata nafasi nyingi za kuweza kushinda mchezo wa leo lakini walishindwa kuzitumia vyema, ikiwemo ya mchezaji wa Kagera Sugar kuzawadiwa kadi nyekundu. Hivyo mpaka refa anamaliza mpira huo timu zote zilitoka uwanjani zikiwa hazijafungana.
Picha na basahama blog
No comments:
Post a Comment