Tume hii iko chini ya Uenyekiti wa Profesa, Mwesiga Baregu, katika siku mbili zilizotangulia ilitoa haki sawa kwa wajumbe kujadili hoja zote zilizomo katika Rasimu ya Katiba. Pichani ni baadhi ya wajumbe wakijadili Rasimu ya Katiba.
Mwenyekiti wa kundi namba "4" Ndugu, Bashiru Madodi akiwa pamoja na Katibu wa kikundi Ndugu,Wema Mwakibibi na Mtunza muda wa kikundi Bi, Estrida Mlinda, akiwasilisha hoja zilizojadiliwa na kundi ambazo zilikuwa ni ibara ya 22 mpaka 53, zilizohusu Haki za binadamu na Wajibu wa raia na mamlaka ya nchi. Na ibara ya 54 mpaka 56, zinazohusu Uraia katika Jamhuri ya Muungano
Mjumbe wa Baraza la Katiba wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Ndugu Yohana Sanga
akichangia hoja za kundi namba nne.
Katibu wa kundi namba nne Ndugu Wema Mwakibibi akifafanua hoja za kundi namba nne
Katika kikao cha Baraza la Rasimu ya Katiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Mjumbe wa Baraza la katiba wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi, Rehema Mwalemba
akichangia hoja katika Baraza la Katiba
Mjumbe wa Baraza la Katiba wa Halmashauri Wilaya ya Rungwe ndugu, Jonathan Msuya
akichangia hoja katika Baraza la Katiba.
Mjumbe wa Baraza la Katiba ndugu, Menrad A. Sangu akichangia hoja katika Baraza la
Katiba.
Kikao cha Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe bado kinaendelea katika ukumbi wa MCHA mjini Tukuyu, tutaendelea kuwajulisha yote yanayoendelea katika kikao hicho baadaye.
Picha zote na taarifa na:- Bashiru Madodi.
No comments:
Post a Comment