Prof. Mwesiga Baregu
Bi, Salma Maolid
Ndugu, Salanus M. Nyimbi
Katika vikao vya kujadili Rasimu ya Katiba wajumbe wamejadili kwa kina rasimu nzima ya katiba na maoni yao kukusanywa na Tume. Wakati wa kuhitimisha Prof. Baregu alisema maoni mengi ambayo yametolewa katika Baraza hili hayajatofautiana sana na maoni ya Mabaraza ya Halmashauri zingine ambazo wamezitembelea.
Pia Prof Maregu amewataka wajumbe wa Baraza la Katiba wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kwa kwenda kuwaelimisha kile ambacho wamekijadili katika kikao hiki cha siku tatu. Mwisho aliwaombea wajumbe ili waweze kuteuliwa kuwemo katika Bunge la Katiba. Picha chini ni matukio mbalimbali ya kikao kizima.
No comments:
Post a Comment