Marehemu Hellena Mwatonoka leo amepumzishwa katika nyumba yake ya milele katika Kijiji cha Ntandabala Kata ya Masoko Wilayani Rungwe. Marehemu Hellena Mwatonoka alikuwa mama mzazi wa Diwani viti Maalumu CCM kutoka Tarafa ya Pakati Mhe. Emmy Mwatonoka. Marehemu Hellena Mwatonoka alizaliwa 10.07.1947. Na kufariki 15.09.2013 amezikwa leo 17.09.2013.
Hili ndilo jeneza lililobeba mwili wa mama yetu Marehemu Hellena Mwatonoka
Diwani Viti Maalumu CCM Emmy Mwatonoka wa pili kulia akiomboleza kifo cha mama yake
Hapa ndipo alipoishi maisha yake ya ndoa Marehemu Hellena Mwatonoka, kwa maana nyingine hapa ndipo palipokuwa nyumbani kwake na ndipo mwili wake ulipopumzishwa milele
Waombolezaji wakiomboleza kabla ya mazishi ya Marehemu Hellena Mwatonoka.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Ndugu Danny Mwakitalu akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Hellena Mwatonoka likiwa tayari kwa mazishi nyumbani kwa Marehemu katika Kijiji cha Ntandabala Kata ya Masoko Wilayani Rungwe.
Basahama Blogspot
No comments:
Post a Comment