Baada ya Serikali ya Marekani kuihusisha al Qaeda, iliamua kuivamia nchi ya Afghanistan na Iraq na kuzishambulia nchi hizo kwa lengo la kumsaka kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden ambaye ndiye aliyehusishwa kupanga njama za kuishambulia Marekani.
Hata hivyo tokea wakati huo ilikuwa ikijulikana kuwa Al Qaeda ni kundi lililoundwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA muongo mmoja kabla ya hapo wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Urusi ya zamani nchini Afghanistan.
Viongozi wakuu wa kundi hilo hususan ukoo wa Bin Laden ulikuwa na uhusiano wa karibu wa kibiashara na baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wakiwemo wa ukoo wa Bush.
Jambo hilo lilisababisha baada ya kutokea kwa tukio hilo Septemba 11.Mashambulizi ya maneno dhidi ya Osama Bin Laden yaliyofuatiwa na uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.
Tangu Marekani ilipoivamia Afghanistan, wasomi wa Marekani walieleza bayana kuwa sera za uingiliaji wa kijeshi za Serikali zilizopita, ndizo zilizosababisha kutokea matukio ya umwagaji damu ya Septemba 11.
Kwa mtazamo wa wasomi na wanafikra hao, kama Serikali zilizopita nchini Marekani zisingeunga mkono ukiukaji wa wazi wa misingi ya demokrasia na haki za binadamu katika pembe mbalimbali duniani na kusababisha maafa kadhaa wakati wa vita ya Ghuba ya Uajemi ya mwaka 1991, huenda magaidi wasingehangaika na Marekani.
Obama anakumbuka
Wakati Wamarekani wanakumbuka na kuadhimisha siku hiyo, Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea maeneo yote ambayo mashambulizi yalitokea.
Katika hotuba yake ya kila wiki alisifu watu waliofanya kazi za uokoaji ambapo walijaribu kuokoa maisha ya wahanga wakati wa mashambulizi hayo.
Mapema mwaka huu, vikosi maalum vya Marekani vilifanikiwa kumwua kiongozi wa Al-Qaida Osama bin Laden huko Pakistan na kutimiza ahadi aliyoitoa rais wa zamani wa Marekani George W. Bush.
Hakuna hotuba
Kwa mara ya kwanza kwenye maadhimisho ya tukio hilo hakukuwepo na hotuba yoyote wakati wa sherehe hizo kutoka kwa wanasiasa.
Chanzo:- Mwananchi.
No comments:
Post a Comment