Timu za Yanga na Mbeya City leo zimetoka sare ya goli 1-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Timu ya Mbeya City ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 50, liliofungwa na Mogani.
Timu ya Yanga ilisawazisha goli katika dakika ya 75 goli lililofungwa Kavumbagu kwa kifua na kumuacha golikipa wa Mbeya City akigalagala bila mafanikio ya kuokoa mpira uliokuwa ukienda wavuni polepole.
Pambano la timu ya Yanga na Mbeya City hii leo limewakumbusha wapenzi wa soka wa jiji la Mbeya na vitongoji vyake enzi za Tukuyu Stars, kwa jinsi mashabiki walivyojaa uwanjani na vituko vya mashabiki waliojaa katika uwanja wa Sokoine, mashabiki wa soka walianza kuingia uwanjani tokea saa nne asubuhi na ilipofika saa nane mchana uwanja wa Sokoine ulikuwa umejaa.
Timu ya Yanga ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuingia uwanjani saa 9:15, timu hii iliingia kwa mbwembwe huku basi lililobeba wachezaji likipita upande walikokuwa mashabiki wa Mbeya City, shabiki asiyejulikana wa Mbeya City alilirushia chupa ya bia basi hilo na kuvunja kioo cha pembeni cha mlango wa dereva na kumjeruhi dereva wa basi hilo, hali iliyoleta mtafaruku mkubwa kwa viongozi wa timu ya Yanga.
Timu ya Mbeya City iliingia uwanjani saa 9:30 jioni. Na kupokewa kwa shangwe na mshabiki wake waliokuwa upande wa kaskazini ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kikosi cha timu ya Yanga ambacho leo kimepambana na timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.
Kikosi cha timu ya Mbeya City ambacho leo kimepambana na timu ya Yanga.
Wachezaji wa Yanga na Mbeya City wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo.
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi kuanza
Wachezaji wa Timu ya Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi katika uwanja wa sokoine tayari kuikabili Mbeya City
Mashabiki wa Mbeya City
Mashabiki wa timu ya Yanga
Basi la Yanga likiwa limevunjwa kioo na mashabiki wa Mbeya City.
Timu ya Yanga ikiwasili katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
Marefa waliochezesha mchezo wa Yanga na Mbeya City wakiwa na makepteni wa timu
Picha zote na Basahama blog.
No comments:
Post a Comment