Wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo wamefanya ukaguzi wa jengo la nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Mpakani katika Kata ya Kikole Wilayani Rungwe. Katika siku zote za ukaguzi wa miradi leo wajumbe walikutana na kimbembe cha kutembea zaidi ya Km 15 kwa miguu. Picha chini ni shughuli nzima ya ukaguzi wa Shule ya Mpakani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula katikati akimuaga Makamu Mwenyekiti Mhe. Ezekiel Mwakota kushoto ili aongoze msafara wa safari ya Km 15 kuelekea Shule ya Msingi Mpakani.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota akiwa amewasili Shuleni Mpakani.
Shule ya Msingi Mpakani kama inavyoonekana katika picha
Darasa jipya la Shule ya Msingi Mpakani kama linavyoonekana katika picha
Jengo la nyumba ya mwalimu ambayo inajengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, jengo hili litakapokamilika litaghalimu Shilingi Milioni 15.
Wanafunzi wa darasa la nne na tano kwa pamoja wakiwa katika darasa moja Shuleni Mpakani, Shule hii ina wanafunzi 20, darasa la nne wanafunzi 15, na darasa la tano wanafunzi 5.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakiwa chini ya mti tayari kwa kupokea taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Mpakani
Mjumbe wa Kamati ya Fedha Mhe. Bashiru Madodi akiwa amefika shuleni Mpakani baada ya mwendo wa Km 15.
Wajumbe wakirudi kutoka shuleni Mpakani
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula akimpokea Mhe. Bashiru Madodi Baada ya kutoka Shuleni Mpakani.
Gari ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ikiwa imekwama.
Gari la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe likipita ndani ya mto.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula akimpokea Mhe. Salome Mwakapala baada ya safari ya Km 15, kutoka Shuleni Mpakani.
Picha zote na Bashiru Madodi
Basahama blogspot
No comments:
Post a Comment