Social Icons

Thursday, 19 September 2013

UKAGUZI WA MIRADI RUNGWE.

Ukaguzi wa miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo umeendelea kwa kukagua miradi ifuatayo, Ujenzi wa nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Lubanda, Ujenzi wa Daraja Bulongwe, Ujenzi wa Ofisi ya Kata Masoko na Ukarabati wa Ofisi ya Kata Bagamoyo.
    
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wakati wa ukaguzi wa miradi.

Daraja la Bulongwe Kata ya Msasani likiwa limekamilika tayari kwa matumizi daraja hili limejengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 48, fedha zote zimetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

Jengo la nyumba ya Mwalimu linalojengwa katika Shule ya Msingi Lubanda Kata ya Ilima, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilitenga Shilingi Milioni 10, kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili.

Jengo la Ofisi ya Kata ya Masoko, jengo hili lilitengewa Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

Jengo la Ofisi ya Kata ya Bagamoyo kama linavyoonekana baadaya kupewa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Shilingi Milioni 10, kwa ajili ya kulifanyia ukarabati mkubwa baada ya kuchakaa.

Afisa mtendaji wa Kata ya Bagamoyo Bi Neema Sarro akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la utawala la Kata ya Bagamoyo kwa wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango.

                                                           Picha zote na Bashiru Madodi
                                                                basahama blogspot.








No comments:

 
 
Blogger Templates